July 3, 2022

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

BAKWATA watoa malekezo mazishi ya watakaokufa kwa COVID-19

Na Irene Clemence

BARAZA la Ulamaa Bakwata Taifa limepitisha mpango maalumu unaohusu taratibu za mazishi ya waislamu wanaokufa kutokana na ugonjwa wa virusi vya COVID 19 ili waweze kupata haki yao ya kuzikwa kwa mujibu wa taratibu za kiislamu.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam leo na Katibu wa baraza hilo Shekhe Hassan Chizenga alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tamko la Baraza la Ulamaa Bakwata Taifa juu ya mwenendo wa COVID 19 na utekelezaji wa ibada hususani Mwezi wa Ramadhani.

Amesema Baraza hilo limefanya mazungumzo na nyanja husika ili kushirikiana na BAKWATA kuunda kamati za maziko zisizo zidi watu saba katika kila Halmashauri kuhakikisha muislamu anayefariki na janga hili anatekeleza mambo yote muhimu kidini katika mazingira salama bila maambukizi.

Pia Baraza hilo limemtaka kila muumini mwenye kikohozi au mafua kusali nyumbani na pale muumini atakapojua wazi kuwa kaathirika au alikuwa karibu na mtu aliyeathirika anapaswa kutambua wazi kuwa ni haramu kwake kuhudhuria msikitini.