May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Asasi za kiraia zatakiwa kushikamana

Na Penina Malundo,timesmajira,Online

RAIS wa Taasisi ya Foundation for Civil Society (FCS),Dkt. Stigmata Tenga amezitaka asasi mbalimbali za kiraia kushikamana kwa umoja na kuhakikisha wanazisemea kazi wanazofanya katika taasisi zao.

Pia amezitaka Asasi hizo kuhakikisha zinaangalia mifumo mbalimbali inayowaongoza ambayo ndio miundombinu ya uwajibikaji katika kazi zao hususani katika kutatua matatizo ya wananchi.

Rai hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki,wakati wa uzinduzi wa Mpango mkakati mpya Taasisi yao katika kufanya kazi na asasi mbalimbali za kiraia.

Dkt.Tenga amesema sekta ya asasi za kiraia inapaswa kujengwa kwani ni miongoni mwa muhimili mkubwa wa maendeleo nchini.

“Tuisemea sekta hii na yale yote ambayo sekta hii inayoyafanya katika jamii,yasemeeni mnayoyafanya ili yajulikane msione aibu yeyote,”amesema

Alisema asasi zinapaswa kutatua matatizo ya wananchi na kusaidia kuyaondoa hilo ndio lengo kubwa la FCS katika dira yake.

wetu ,tutoe baries zilizopo kwa watu ambazo zipo tujikite hapo katika hilo,

“Tujenge uwajibikaji katika misingi ya ubinadamu na utu bila kujalisha kunanini bali kuwagaia na wenzetu,matatizo ambayo sekta ya kiraia nchini yanayopitia ambayo yanahitaji kutatuliwa ni matatizo yanayojikita katika mifumo,”amesema

Aidha amesema hawapaswi kutatua matatizo kwa mbinu zile zile za zamani ambazo sio mbinu za kujenga mifumo bali ni mbinu za kutoa huduma.

“Tusipoangalia hivyo tutazidi kuona hizo mbinu zinaongezeka na kuwa kubwa sana na kuhakikisha wanaangalia mifumo ambayo ndio miundombiniu ya uwajibikaji katika taasisi,”amesema

Kwa Upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa FCS,Francis Kiwanga alisema wamezindua mpango mkakati mpya wa FCS ambao unalenga kushuka chini hususani vijijini katika kuwasaidia wananchi.

Amesema kupitia mpango huo taasisi yao itaendelea kufanya kazi na asasi mbalimbali za kiraia ambao ndio wadau wao muhimu katika kuwafikia wananchi.

Amesema salfasa ya taasisi yao inaamini kuwa umasikini,hali ya kutokuwa na haki katika jamii,hali ya ukandamizaji watu wengine ni tatizo kubwa na ni adui wakubwa wa maendeleo.

Amesema katika rasilimali zao takribani asilimia 90 inakwenda vijijini kuhudumia wananchi .“Rasilimari zetu tunavyogawa kila mwaka asilimia 90 inakwenda vijijini tunaamini waliopo Dar es Salaam ,taasisi nyingi zinaweza kufanya kazi na watu wengine kokote duniani,kuliko waliopo vijijini”amesema

Pia amesema katika mpango wao wanazingatia usawa wa kijinsia,kufanya kazi na wadau wao kuwapa heshima inayostahili na kuwaheshimu kwani wao ni wabia wao ambao wanasauti kubwa .

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Asasi za kiraia,Dkt.Richard Samabiga ameipongeza FCS kwa hatua hiyo ya kuzindua mpango mkakati huo ambao unaonyesha dira ya kusaidia wananchi katika maeneo mbalimbali.

Amesema mpango huo unaleta matumaini makubwa kwa asasi za kiraia katika kufanya kazi zao za kusaidia wananchi.