Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Manyoni
MGOMBEA ubunge jimbo la Manyoni Mashariki kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Pius Chaya amesema miongoni mwa vipaumbele vyake pindi akichaguliwa na wananchi kuwa Mbunge wa Jimbo hilo ni kujenga hosteli za watoto wa kike ili kupunguza mimba kwa wasichana shuleni.
Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu katika ofisi ya msimamizi wa uchaguzi wilayani humo ,Dkt.Chaya amesema matukio ya wasichana kupata mimba na kukatisha masomo yao yanasababishwa na ukosefu wa hosteli lakini pia kukosa mazingira mazuri ya kusomea wawapo nyumbani.

“Mimba mashuleni na ukosefu wa hosteli bado ni tatizo,hili nitalifanyia kazi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali”amesema Dkt.Chaya
“ Hapa ni mjini tunahitaji kuwa na barabara za lami lakini tuna barabara moja kubwa sana ya kutoka Manyoni kwenda Sanza-Heka-Chikola
hadi Dodoma ,mipango niliyonayo ni pamoja na kuunganisha barabara hiyo ya wilaya ya Manyoni na Mkoa wa Dodoma.”alisema Dkt.Chaya

More Stories
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi