Na Martha Fatael,TimesMajira,Online Moshi
JESHI la Polisi mkoani Kilimanjaro limewataja watu wanne waliojeruhiwa na Chui anayedhaniwa kutoka Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) na baadaye kuvamia zahanati ya Huruma iliyopo wilaya ya Hai mkoa wa humo.
Taarifa zinaeleza kuwa mnyama huyo alidhibitiwa kwa ushirikiano baina ya askari wa wanyapori (TAWA), KINAPA pamoja na jeshi la polisi bila ya kuleta madhara zaidi.
Taarifa ya Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Simon Maigwa, imewataja majeruhi kuwa ni Jesca Nnko (21),Emmanuel Usara (37), Urusula Cosmas (26) na Maliki Sakia(31) wote wakazi wa Bomang’ombe wilaya ya Hai.
Maigwa alisema majeruhi wanaendelea vyema Katika hospitali ya wilaya ya Hai wakiwa chini ya uangalizi wa madaktari ili pia kufanyiwa uchun…
More Stories
Watatu mbaroni kwa tuhuma za mauaji wakigombania shamba
Ng’ombe 10 wamekufa kwa kupigwa na radi
Rukwa waanzisha utalii wa nyuki