April 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wanafunzi viziwi kuomba serikali iwasaidie

Na Penina Malundo,timesmajira,Online

JUMUIYA  ya Wanafunzi wa Buguruni Viziwi  (BUGURUNI VIZIWI ALUMN),imeiomba  serikali na wadau mbalimbali nchini kujitokeza kwa wingi na kusaidia changamoto wanazokabiliana nazo.


Miongoni mwa changamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja na kutokuwa na Ofisi ya kufanyia shughuli zao pamoja na miundombinu mbalimbali ya kuwawezesha katika kazi zao.


Akizungumza hayo hivi karibuni mkoani Dar es Salaam,wakati wa maadhimisho ya wiki ya Viziwi Duniani, Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Jumuiya hiyo,Subira Upurute amesema kundi la Viziwi ni miongoni mwa kundi ambalo linasahaulika na jamii yake kuona kama  hawana haki sawa na wengine.


Amesema wamekuwa wakijitahidi kushirikiana na wadogo zao wanasoma shule hiyo kufanya matukio mbalimbali  ili jamii ielewe kwamba ulemavu wao sio kushindwa.

 
“Katika Kuadhimisha siku wiki ya maadhimisho ya viziwi,tuliamua kukutana na wadogo zetu wanasoma shule ya Buguruni viziwi na kufanya usafi kwa lengo la utunzaji wa mazingira,”amesema Upurute


Amesema mbali na kufanya usafi huo pia waliweza kujadili hatima ya Shule yao ikiwemo kutatua changamoto zinazowatatiza ikiwemo kuchangiana  ili kufanikisha ujenzi wa Karo la kufulia nguo.


“Huu ni mwaka wa nne tangu tuanze Jumuiya yetu ya Buguruni viziwi Alumn na kuhakikisha tunatatua changamoto zinazotukabili ili wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo wasikumbane nazo,”amesema

 
 Upurute amesema Jumuiya yao pia inakabiliwa na Changamoto mbalimbali kama   ikiwemo ofisi, vitendea kazi hatuna na kuwapatia  wanachama  elimu ya ushirikishwaji katika  mambo mbalimbali ya kijamii.


Kwa Upande wake  Mkurugenzi wa Chama cha kuhudumia Viziwi Tanzania(TSD) Yasini Mawe amewapongeza  UMOJA  wanafunzi  hao kwa kujitoeza na kuwakumbuka wadogo zao katika shule hiyo.


Amesema umoja huo ulianzishwa mwaka 2015 katika shule chini ya Chama chao na kuwaunganisha wanafunzi wote waliosoma katika shule hiyo.


Naye Mmoja wa Wanafunzi hao,Joseph Hiza alisema huo ni mwanzo kwao na wanatarajia kufanya mambo mengi katika shule hiyo kwa lengo la kuonyesha ushirikiano kwa wanafunzi wenzake.

Mwishooo

ReplyReply allForward