Na.Mwandishi wetu,Timesmajira
Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Nishati na Petroli wa Jamhuri ya Senegal,Dkt. Elhadji Abdourahmane Diouf, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kati ya Tanzania na Senegal katika maendeleo ya sekta ya nishati.
Mazungumzo hayo yamefanyika Agosti 6, 2026, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam, ambapo viongozi hao walijadili fursa mbalimbali za ushirikiano zitakazochochea maendeleo ya sekta hiyo katika nchi zote mbili.

Miongoni mwa maeneo yaliyojadiliwa ni kubadilishana uzoefu na utaalamu, mafunzo kwa wataalamu wa sekta ya nishati, matumizi ya teknolojia katika utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia, pamoja na kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya nishati.
Pande hizo mbili zilisisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano wa karibu ili kukuza uwekezaji, kuongeza ufanisi wa sekta ya nishati na kuchangia maendeleo ya uchumi wa Tanzania na Senegal.
Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi, Dkt. James Mataragio.



More Stories
T-CAMS yaleta mapinduzi sekta ya uwakala wa forodha
Mafuta ya zabibu yavutia Nanenane
Nanauka apongeza Kariakoo Kwa kuwezesha vijana Kibiashara