Na Mwandishi wetu
MWENYEKITI wa Umoja wa Chama cha Mapinduzi ( UWT) Taifa, Mary Pius Chatanda (MCC), ameendelea na ziara yake ya siku tatu mkoani Songwe kwa kufanya mkutano wa ndani uliowakutanisha wanachama wa UWT, wanachama wa CCM na wananchi wa Wilaya ya Songwe tarehe 3 Agosti 2026.
Akizungumza katika mkutano huo, Chatanda aliwasilisha salamu maalum kutoka kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa. Aidha, aliwashukuru wananchi na wanachama kwa ushiriki wao katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 na kuwapongeza kwa kuendelea kulinda na kudumisha amani, umoja na utulivu nchini.
Vilevile, Chatanda aliwahimiza wanachama na wananchi kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutambua juhudi zake katika kuwaletea maendeleo na kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi.
Ziara hiyo inaratibiwa na Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UWT Taifa na inahusisha mikoa 12 ya Tanzania Bara. Lengo la ziara hiyo ni kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025–2030 pamoja na kutathmini uhai na uimara wa Chama na Jumuiya zake.

More Stories
Mikopo asilimia 10 yainua wanawake Tunduma kibiashara
UDSM yabuni bidhaa kwa nazao ya nyuki
Airtel yaimarisha ushirikiano wa Airtel Business Monthly Mug Tournament