May 6, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Chanjo ya polio awamu ya pili kuwafikia 176,644

 

Na Judith Ferdinand,Mwanza

AWAMU  ya pili ya chanjo dhidi ya polio kwa watoto wenye mwenye umri chini ya miaka 10,linatarajia kufanyika kwa siku nne Mei 7 hadi 10,2026,ambapo Halmshauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza inatarajia kuwachanja takribani watoto 176,644.

Zoezi la utoaji wa chanjo ya polio awamu ya pili litahusisha watoto wote waliopatiwa chanjo awamu ya kwanza na wale  na ambao hawakupatiwa.

Hivyo ili kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa ufanisi halmshauri hiyo kupitia idara ya afya imetoa elimu ya chanjo ya polio na madhara yatokanayo na ugonjwa huo kwa makundi mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, wazee maarufu, wamiliki wa shule binafsi na viongozi wa vijana.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma wa Halmashauri ya Manispaa  ya Ilemela Kalunde Gisema,amesema mafunzo hayo  yakilenga kutoa uelewa kwa jamii kupitia viongozi hao juu ya umuhimu wa chanjo ya polio noVP2 awamu ya pili kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 10.

“Hawa ni watu muhimu  wanaoaminika na kusikilizwa katika jamii,hivyo kupitia mafunzo hayo tunaamini sehemu kubwa itapata uelewa juu ya umuhimu wa chanjo ya polio awamu ya pili.Pia itahamasikana  watoto wao  kupata chanjo hivyo kuwakinga na virusi vinavyoeneza ugonjwa wa polio,”amesema Kalunde.

Kwa upande wake Sheikh wa Wilaya ya Ilemela,Abdulmalick Juma,ameahidi  kutoa elimu hiyo waliopata kwa jamii kuhusu umuhimu wa chanjo hiyo  kwa watoto na kuhamasisha wazazi kuhakikisha  watoto wao wanapata  chanjo ya polio. 

Katibu wa soko la Kiloleli wilayani Ilemela mkoani Mwanza,Happynes Lakate,amesema atahakikisha anawahamasisha wafanyabiashara wa sokoni hapo na masoko jirani wenye watoto wa umri chini ya miaka 10, kuhakikisha wanapata chanjo hiyo  ili kuwakinga na ugonjwa wa polio.

Ambapo amesema  mtoto akipata maradhi mzazi hataweza  kufanya biashara ajatjikita zaidi kuhakikisha  mtoto wake anapata tiba na hivyo uchumi kushuka.