Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Oline, Kigoma
KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amepata ajali ya gari akiwa njiani akitokea Kata ya Kalya kuelekea Lukoma kwenye kampeni katika Jimbo la Kigoma Kusini.
Taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari iliyotolewa na Afisa Habari ACT-Wazalendo, Arodia Peter, ilieleza kuwa ajali hiyo ilitokea jana ambapo Zitto alikuwa na watu watano kwenye gari yake.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo Zitto na watu hao ote wako salama ingawa walipata majeraha na wanahisi maumivu makali. Taarifa hiyo ilieleza kwamba baada ya ajali hiyo walipata huduma ya kwanza kwenye eneo la ajali baadaye walipelekwa Kituo cha Afya cha Kalya kilichopo Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.
Mwisho
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Jay-Z aunganishwa na P Diddy kwa kumdhalilisha binti wa miaka 13
Rais Samia afanya uteuzi