March 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina

Ziara ya usiku ya Waziri Mpina yamtumbua kigogo

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ametengua uteuzi wa Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Dkt. Sophia Mlote kufuatia kutoridhishwa na utendaji wake wa kazi.

Mabadiliko hayo yamekuja siku chache baada ya Waziri Mpina kufanya ziara ya kushtukiza saa 10 usiku katika eneo Ubungo wanakouza maziwa wajasiriamali wadogo na kupokea malalamiko ya wajasirimali hao kuharibiwa maziwa yao kwa kuwekewa rangi na Mafuta ya taa na baadhi ya maofisa wa Bodi ya Maziwa .

Aliyekuwa Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa Tanzania, Dkt. Sophia Mlote

Hata hivyo Waziri Mpina ameagiza maofisa wa Bodi ya Maziwa kusitisha mara moja operesheni ya kuharibu maziwa ya wananchi na kutaka hatua za haraka zichukuliwe kuwaelimisha namna bora ya kufanya biashara hiyo badala ya kuchukua uamuzi wa kuharibu maziwa yao kwa rangi na mafuta ya taa.

Kwa mujibu wa Taarifa kwa Umma iliyotolewa na Kaimu Mkuu wa Kitengo Serikalini, Elibariki Mafole imesema uamuzi uliofanywa na Waziri Mpina ni kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa chini ya Sheria ya Maziwa namba 8 ya mwaka 2004.

Taarifa hiyo imesema kuwa uteuzi wa Msajili wa Bodi ya Maziwa Utafanyika hapo baadae.

Hata hivyo baada ya Waziri Mpina kufika eneo hilo la Ubungo alihoji hatua ya kuharibu maziwa ya wananchi kwa kuweka rangi na mafuta ya taa iliyofanywa na Bodi ya Maziwa ulizingatia Kanuni gani jambo ambalo maofisa wa Bodi hiyo walioshindwa kuonesha kifungu kinachowapa mamlaka ya kupima maziwa kwa macho na kuweka mafuta ya taa.

Mmoja wa wafanyabiashara wa maziwa, Ester Elius amesema zoezi hilo lililofanywa la kuwawekea mafuta ya taa rangi kwenye maziwa limewapatia hasara kubwa na kuomba serikali kuwasaidia mikopo ili waweze kukidhi matakwa ya kisheria yanayotakiwa na bodi hiyo badala ya

Hivyo Waziri Mpina ameagiza Mratibu wa Dawati la Sekta Binafsi la Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Stephen Michael kukutana na wajasirimali hao ili kutambua mahitaji yao ya kifedha na kuwaunganisha na Taasisi za kifedha kwa ajili ya kupatiwa mikopo ili waweze kufanya biashara zao kwa tija.

Ofisa wa Bodi ya Maziwa, Justa Kashumba amesema hatua walizochukua kuharibu maziwa hayo zipo kwa mujibu wa kanuni huku akishindwa kumuonesha kanuni iliyotumika Waziri Mpina.