April 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri wa Nishati,Dkt Medard Kalemani(mwenye miwani) akitoka kukagua ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Nguruka, Kilichopa katika kijiji cha Mganza Wilaya ya Uvinza,Mkoani Kigoma Juni 27,2020.

TANESCO yapewa siku 5 kulipa fidia Kidahwe

Na Hafsa Omar, Kigoma

Waziri wa Nishati,Dkt Medard Kalemani ametoa siku tano kwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kulipa fidia kwa wananchi  wa Kidahwe waliopisha ujenzi wa kituo cha kupoza  umeme(substation) cha Kidahwe kilichopo katika Kijiji cha Kidahwe, Kata ya Kidahwe Wilaya ya Kigoma vijijini, Mkoani Kigoma.

Waziri wa Nishati,Dkt Medard Kalemani akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kufika kukagua ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Nguruka, Kilichopa katika kijiji cha Mganza Wilaya ya Uvinza,Mkoani Kigoma Juni 27,2020.

Agizo hilo amelitoa 27 Juni 2020, wakati akiwa kwenye uzinduzi wa kuanza malipo kwa wananchi ambao wameridhia kutoa ardhi yao kwaajili ya ujenzi wa kituo cha Kupoza umeme cha Kidahwe.

Akizungumza kwenye tukio hilo amesema, zaidi ya shilingi milioni 700 zipo tayari kwaajili ya malipo ya wananchi 411 na kuwataka TANESCO kuanza mara moja kuwalipa wananchi hao na kuwapa siku tano tu kumaliza zoezi hilo.

“Niliacha maelekezo kwa waatalamu wetu kufanya kazi mbili, kazi ya kwanza ilikuwa kuhakikisha wananchi wanaozunguka maeneo ya mradi ambao wanapitiwa  mradi wafanyiwe tathimini na kulipwa fidia zao na jambo hili tayari limeanza kufanyiwa kazi na jambo la pili ni kuanza matayarisho ya ujenzi wa mradi mkubwa huu,”amesema Dkt Kalemani.

Waziri wa Nishati,Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kidahwe,kata ya Kidahwe Wilaya ya Kigoma vijiji, Mkoani Kigoma,wakati akiwa kwenye uzinduzi wa kuanza malipo kwa wananchi ambao wameridhia kutoa ardhi yao kwaajili ya ujenzi wa kituo cha Kupoza umeme cha Kidahwe, Juni 27,2020.

Aidha, Dkt Kalemani amewashukuru wananchi wa eneo hilo kwa kutoa maeneo yao kwaajili ya ujenzi wa kituo hicho kikubwa  chenye uwezo wa kuzalisha umeme wa Kv 400, umeme huo ambao  unatarajiwa kuondoa kero ya upatikanaji wa umeme Mkoani humo.

Dkt Kalemani amewataka wananchi watakaolipwa fidia hiyo kuzitumia vizuri fedha zao vizuri  kwa kununua maeneo mengine na kujiendeleza kiuchumi.

“Mtakao lipwa fedha zenu msije mkazitumia vibaya hiyo hela halafu mkarudi tena TANESCO kudai hela nyengine hakuna hela nyingine hela ni hiyo hiyo utakayolipwa,” amesema.

Vilevile, amewataka TANESCO kuanzia tarehe 5 Julai waanze mara moja ujenzi wa kituo hicho, ili wananchi wa Kigoma waanze kupata umeme wa uhakika ambao utawasaidi kujenga uchumi wa Mkoa huo.

Wananchi wa wananchi wa kijiji cha Kidahwe,kata ya Kidahwe Wilaya ya Kigoma vijiji, Mkoani Kigoma, wakiwa na furaha mara baada ya Waziri wa Nishati,Dkt Medard Kalemani kuwatangazia kuwa ndani ya siku tano wote watakuwa wamelipwa malipo yao, Juni 27,2020.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Emmanuel Maganga amewashukuru wananchi wote waliotoa maeneo yao kwaajili ya maendeleo ya Mkoa huo na amewahakikisha pesa zipo tayari kwaajili ya malipo yao.

Pia, amewatahadharisha wale wote watakaolipwa fidia hawataruhusia kuyatumia tena maeneo hayo kwani maeneo hayo yatakuwa ni mali ya Serikali kwasababu watakuwa tayari Serikali imeyalipia.

Waziri wa Nishati,Dkt Medard Kalemani(wa kwanza kushoto) akiwa pamoja na uongozi wa Mkoa wa Kigoma na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kidahwe wakiwa wameshika mfano wa hundi itakayolipwa kwa wananchi wa kijiji cha Kidahwe,kata ya Kidahwe Wilaya ya Kigoma vijiji, Mkoani Kigoma, Juni 27,2020.

Katika ziara yake hiyo mkoani Kigoma, Dkt Kalemani pia ametembea kwenye kituo cha kupoza umeme cha Nguruka kilichopo katika kijiji cha Mganza na kuwataka TANESCO kumaliza ujenzi wa kituo hicho Julai mwaka huu.

Waziri wa Nishati,Dkt Medard Kalemani(mwenye miwani) akiondoka kwenye uzinduzi wa kuanza kwa malipo ya wananchi ambao wameridhia kutoa ardhi yao kwaajili ya ujenzi wa kituo cha Kupoza umeme cha Kidahwe,mara baada ya kumaliza kwa tukio hilo, Juni 27,2020.