May 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Yanga SC, UNICEF waingia mkataba

Zuhura Mohamed, Timesmajira Online

Klabu ya YangaSC leo Oktoba 18, 2022 imeingia mkataba wa miezi sita na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto – UNICEF kwa ajili ya kuongeza uelewa kwa umma kuhusu chanjo ya UVIKO-19 na uhamasishaji kuhusu virusi vya Ebola.

Kwa mara ya kwanza klabu ya Yanga, kuingia katika historia ya vilabu hapa Afrika Mashariki.

Akizungumza na waandishi wa habari leo katika Hotel ya Serena jijini, Dar e Saalaam Rais wa Yanga Injini Hersi Saidi alisema Yanga SC itakua na jukumu la kwenda kutoa elimu na misaada kwa jamii ya watu wenye mahitaji maalumu, na kwa wathirika wa magonjwa ya UVIKO-19 na Ebola.

Kupitia Mkataba huO, Klabu hiyo Kongwe Afrika Mashariki na Kati, inakwenda kuunga mkono jitihada za Serikali kupambana na magonjwa haya makubwa mawili kwa sasa.

“Gharama zote za kutekeleza mradi huu zinasimamiwa na UNICEF, kuna ada ambayo UNICEF inailipa Yanga katika kutekeleza miradi hii,”

“Tunashirikiana na UNICEF ili kila Mwanachama, Mpenzi na Mshabiki wa Yanga na Vilabu vingine wapate maarifa na uelewa kuhusu chanjo ya UVIKO-19.

“Ni jukumu letu kama Klabu kuunga mkono juhudi zitakazotuwezesha kushinda UVIKO-19 na Ebola,”
“Tunajulikana kama timu ya Wananchi. Falsafa yetu ni kuwa sehemu ya suluhisho la changamoto zinazowakabili Wananchi,” amesema Rais wa Yanga SC Hersi Said wakati wa kusaini mkataba huo

Naye mwakilishi wa UNICEF, Fatimata Baladi amesema klabu ya Yanga imewaonesha umuhimu mkubwa kwenye sekta ya michezo katika kukabiliana na changamoto katika sekta za afya.

“Yanga SC imetuonyesha umuhimu wa michezo kwenye kutatua changamoto zilizopo katika sekta ya afya ushirikiano wetu utasaidia zaidi ya mashabiki milioni 25 wa soka nchini Tanzania kupata taarifa sahihi kuhusu chanjo ya UVIKO-19 na virusi vya Ebola ili waweze kujilinda,” amesema Baladi.