May 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Benzena anayakuwa tuzo ya Ballon
d’Or, Mane ashika nafasi ya pili

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

Mshambuliaji wa Real Madrid na Ufaransa, Karim Benzema ameshinda tuzo ya Ballon d’Or, tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka huu kwa mara ya kwanza.

Benzema alifunga mabao 44 katika michezo 46 alipoisaidia Real kushinda Ligi ya Mabingwa na Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) msimu wa 2021-22.

Akizungumza baada ya kushinda tuzo hiyo, Benzema alisema najisikia furaha sana kuona nanyakua Tuzo hiyo kwani ilikuwa ndoto yake tangu utotoni.

“Siku zote nilikuwa na mawazo kwamba lolote linawezekana, nilipokuwa sipo katika timu ya Ufaransa sikuacha kufanya kazi kwa bidii.

‘Kwa kweli ninajivunia safari yangu hapa. Haikuwa rahisi, ulikuwa wakati mgumu na pia kwa familia yangu. Kusimama hapa leo kwa mara ya kwanza, nina furaha kwa kazi yangu na nitaendelea,” amesema Benzema.

Benzema alikua mchezaji wa tisa wa Real Madrid kutwaa tuzo hiyo tangu 2000 na Mfaransa wa tano pekee kuwahi kushinda taji hilo.

Wachezaji wengine walioshika kumi bora, kwa mpangilio wa kushuka ni, Erling Haaland, Luka Modric, Vinicius Jr, Thibaut Courtois, Kylian Mbappe, Mohamed Salah na Robert Lewandowski.