April 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Ndalichako akutana na kuzungumza na viongozi umoja wa watu wenye ulemavu waendesha bajaji (UWAWABADA)

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amekutana na kuzungumza na Uongozi wa Umoja wa Watu wenye Ulemavu waendesha Bajaji kutoka Mkoa wa Dar es Salaam (UWAWABADA) wametembelea katika ofisi yake jijini Dodoma kwa lengo la kubadilishana mawazo na kujadiliana kwa pamoja changamoto mbalimbali zinazowakabili katika sekta hiyo.

Aidha, Katika kikao hicho viongozi hao na wajumbe wa UWAWABADA wametoa pongezi zao kwa Waziri pamoja na Ofisi yake kwa namna wanavyo shughulikia masuala mbalimbali yanayowakabili Watu wenye Ulemavu ili kuimarisha ustawi wa kundi hilo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akiwa katika mazungumzo na Viongozi wa Umoja wa Watu Wenye Ulemavu waendesha Bajaji Mkoa wa Dar es Saalam (UWAWABADA) walipomtembelea katika ofisi yake iliyopo Jengo la OSHA Jijini Dodoma, Juni 28, 2022.
Sehemu ya Viongozi na Wajumbe wa Umoja wa Watu Wenye Ulemavu waendesha Bajaji Mkoa wa Dar es Saalam wakisikiliza maelezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani).
Mwenyekiti wa Umoja wa Watu Wenye Ulemavu waendesha Bajaji Mkoa wa Dar es Saalam (UWAWABADA), Bw. Paul Majige akieleza jambo wakati wa kikao hicho na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako walipomtembelea katika ofisi yake iliyopo Jengo la OSHA Jijini Dodoma, Juni 28, 2022.
Mjumbe wa Umoja wa Watu Wenye Ulemavu waendesha Bajaji Mkoa wa Dar es Saalam (UWAWABADA), Bi. Evodia Nchimbi akichangia jambo wakati wa kikao hicho.
Katibu wa Umoja wa Watu Wenye Ulemavu waendesha Bajaji Mkoa wa Dar es Saalam (UWAWABADA), Rebman Materu akifafanua jambo wakati wa kikao hicho na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako walipomtembelea katika ofisi yake iliyopo Jengo la OSHA Jijini Dodoma, Juni 28, 2022.