December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Chana akutana na Balozi wa China nchini Tanzania

Na mwandishi wetu, TimesMajira Online

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb)akutana na Balozi wa China nchini Tanzania , Mhe. Chen Mingjian Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) akimuonyesha na kumpa maelezo Balozi wa China nchini Tanzania , Mhe. Chen Mingjian kuhusu sahani za zamani za kutoka china zilizohifadhiwa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam.
Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Chen Mingjian akiuliza swali kutokana na maelezo aliyapata ya uhifadhi wa mikisanyo na hitoria Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) akimkabidhi Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Chen Mingjian kitabu cha historia ya mikusanyo yenye asili ya China ilioyopatikana Tanzania na inayohifadhiwa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni alipotembelea Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) na Balozi wa China nchini Tanzania Mhe. Chen Mingjian katikati, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam.