May 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TANROADS yakamilisha miradi 14 yenye gharama ya shilingi Trilioni 1.37 kwa kipindi cha Serikali awamu ya sita

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.

WAKALA wa Barabara Tanzania(TANROADS)imesema imefanikiwa kukamilisha jumla ya miradi 14 yenye urefu wa kilometa 883 katika kipindi cha wa awamu ya sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wenye gharama ya sh.Trilioni 1.37.

Hayo yameelezwa na Mtendaji Mkuu wa TANROADS,Mhandisi Rogatus Mativila wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu majuku na vipaumbele vyake kwa mwaka wa fedha 2022/23.

Mha.Mativila ametaja miradi hiyo iliyokamilika kuwa ni Miradi ya barabara ya Kidahwe – Kasulu (km 63) – Mkoa Kigoma
Nyakanazi – Kibondo (Kabingo) (km 50) – Mkoa Kigoma, Mbinga – Mbamba Bay (km 66), Ruvuma, Njombe – Moronga Section (km 53.9), Njombe, Moronga – Makete Section (km 53.30), Njombe, Makutano – Natta (Sanzate) Section (km 50) – Mkoa wa Mara
,Waso – Sale Jct Section (km 49), Arusha

Mingine ni Kikusya – Ipinda – Matema (39.10km),Mbeya,Chunya – Makongolosi (km 39), Mbeya,Lot 1: Usesula – Komanga Section and Sikonge Spur Road (km 115.50), Tabora,Lot 2: Komanga – Kasinde Section) and Iyonga Spur Road (km 112.80), Katavi, Lot 3: Kasinde – Mpanda Section and Urwira Town Section (km 108.00), Katavi, Mpemba – Isongole Road (km 50.30), Songwe na Mpanda – Kibo – Usimbili (km 37.65)

Pia ametaja na Miradi ya Madaraja Makubwa iliyokamilika kuwa ni Tanzanite Bridge, Dar es Salaam, (km 1.03),Ruhuhu bridge along Kitai – Lituhi road in Ruvuma Region (m 98),Magara Bridge in Manyara region (m 84), Mara Bridge in Mara Region (m 940), Msingi Bridge, Singida (m 100);
(vi) Sibiti Bridge, Singida (m 82) na Wami Bridge, Pwani (m 514)

Vilevile Mha.Mativila amesema kuwa jumla ya miradi 44 ya barabara yenye urefu wa kilometa 1,523 yenye gharama ya Shilingi Trilioni 3.8 ipo katika hatua mbali mbali ya ujenzi nchi nzima.

“Miradi hii inahusisha miradi inayogharamiwa na Serikali kwa kutumia fedha za ndani na inayogharamiwa kupitia Washirika mbalimbali wa Maendeleo,

“Aidha, mradi mkubwa wa ujenzi wa Kiwanja cha ndege cha Msalato unaojumuisha ujenzi wa njia ya kurukia ndege na majengo ya abiria unaendelea chini ya ufadhili wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) kwa gharama ya Shilingi Bilioni 360,”amesema.

Pia Mha.Mativila ameeleza kuwa
Miradi ya barabara 62 iko katika hatua mbalimbali za manunuzi kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami.

“Barabara hizi zinajumuisha miradi inayogharamiwa na Serikali kwa kutumia fedha za ndani pamoja na fedha kutoka kwa Washirika wa maendeleo,”amesema.

Aidha,amesema kuwa Miradi ya Madaraja Makubwa mitatu (3) ambayo ujenzi unaendelea  ipo katika hatua mbalimbali ya utekelezaji kwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 701.

Miradi mingine ya Madaraja Makubwa sita  ambayo usanifu wa kina umekamilika ambayo ni Simiyu (barabara ya Mwanza – Musoma), Bwawa la Mtera (barabara ya Iringa – Dodoma), Mzinga (barabara ya Dar es Salaam – Kibiti), Mitomoni (Ruvuma),na Daraja la Jangwani.

Ametaja miradi mingine kuwa ni Miradi ya EPC+ F ambayo Wizara ya Ujenzi kupitia TANROADS imeanza utekelezaji wa Miradi ya EPC + F yenye urefu wa kilometa 2,533km. Makampuni yaliyokuwa “shortlisted’ yamealikwa tarehe 22 Septemba, 2022 kuwasilisha zabuni tarehe 22 Novemba, 2022.

“Miradi hiyo ni Kibaha – Mlandizi Chalinze – Morogoro (km 205) Expressway,  Kidatu – Ifakara – Lupiro – Malinyi – Kilosa Mpepo – Londo – Lumecha/Songea (km 512),Arusha – Kibaya – Kongwa Road (km 493), Handeni – Kiberashi – Kijingu – Njoro – Olboroti – Mrijo Chini – Dalai – Bicha – Chambolo – Chemba – Kwa Mtoro – Singida (km 460), Igawa – Songwe – Tunduma (km 218), Masasi – Nachingwea – Liwale (km 175),Karatu – Mbulu – Hydom – Sibiti River – Lalago – Maswa (km 389) na  Mafinga – Mtwango (Km 81)

Mha.Mativila pia ametaja Jumla ya miradi 43 ya barabara yenye urefu wa kilometa 2,021.04 na gharama ya Shilingi Bilioni 9.6 ipo katika hatua mbali mbali za upembuzi yakinifu na usanifu.

“Katika mwaka wa fedha 2021/22, kati ya Julai 2021 hadi Mei 2022, jumla ya mikataba 20 inayohusisha miradi ya ujenzi wa Barabara na Viwanja vya Ndege inayogharimiwa moja kwa moja na fedha za ndani na mingine kugharimiwa kwa fedha za Washirika wa Maendeleo ilisainiwa,

“Mikataba ya ujenzi wa barabara zenye jumla ya km 582.455 imesainiwa na mikataba ya ujenzi wa Kiwanja cha ndege Msalato na kumalizia jengo la Kiwanja cha ndege Songwe pamoja na mizani ya Rubana ilisainiwa na gharama ya miradi yote 20 ni Shilingi Bilioni 1,460.84