April 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wazazi washauriwa kuacha kutoza mahari kubwa inachangia watoto kutoolewa

Na Patrick Mabula ,Kahama

OFISA maendeleo ya wazazi wa Halmashauri ya Mji wa Kahama,Mary Chima imeitaka jamii hasa zakifugaji kuacha kuwageuza watoto wao kama kitegauchumi wanapotaka kuolewa kwa kutoza mahari kubwa hali inayofanya washindwe kuolewa na kujiingiza katika biashara halamu ya ngono na kuzaa bila utaratibu.

Chima amesema kuwageuza watoto wa kike kama kitega uchumi kwa kutoza mahari kubwa ni moja ya sababu ya kuwepo kwa watoto wengi wasiokuwa na baba,wanaolelewa na bibi zao kutokana na kuzaliwa nje ya ndoa kutokana na wazazi kwa tamaa ya mali kupanga ghalama kubwa ya mahali inayowashinda vijana waoaji.

Akiongea katika kikao cha siku moja ya kujadili namna ya kutunga sheria ndogondogo zinatakazo walinda wanawamke na mtoto kike dhidi ya mila na desturi potofu zinazopelekea ukatili wa kijinsia iliyoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Huheso Foundation kwa ufadhili wa The Foundation for Civil Society(FCS) amesema sheria hizo zitasaidia jamii pamoja na elimu inayoendelea kutolewa kwao.

Chima amesema moja ya mira iliyopitwa na wakati ni kwa baadhi ya wazazi , walezi hasusa jamii ya kifugaji ya kutoza mahari kubwa ya fedha na mifugo kwa wanawake wanapochumbiwa kwa lengo la kuondokana na umasikini imekuwa ikichangia kwa asilimia kubwa vijana kushindwa kumdu gharama hizo na kusababisha mabinti kujiingiza kwenye biashara haramu ya ngono na kupata ujauzito wakiwa nyumbani.

“Ndugu zangu jamii yote tunapasawa kuangalia sana kuhusu swala la mahali kubwa pale mabinti zetu wanapochumbiwa kuolewa kwa sababu vijana wengi wanashindwa kuoa baada ya kuelezwa ghalama kubwa na kusababisha watoto wa kike kujiingiza kwenye biashara haramu na kuzaa watoto na kuwatelekeza” amasema Chima.

Ofisa Ustawi wa jamii wa almashauri ya mji wa Kahama, Abrahaman Nuru alisema wazazi na walezi katika familia zao inawajibu wa kubadirika na kupinga mila na desturi kandamizi kwa mtoto wa kike zilizopitwa na wakati katika kuwalinda na ukatili wa kijinsia na kuwashirikisha katika mipango yote kwa usawa.

Kwa upande wake ofisa sheria wilayani hapa,Joel Mracha amesema kuwa, mwanamke anapofiwa na mwenza wake anahaki ya kuisha popote,lakini baadhi ya makabila yamekuwa yakimtafutia mridhi ambae ni mdogo wa marehemu na kuanza kunyanyasiaka na wengine kuchukua jukumu la kukimbia familia.

Macha alitoa wito kwa mashirika binafsi mbalimbali yanayojishughulisha na kupambana na ukatili wa kijinsia kwa watoto wa kike kuendelea kutoa elimu kwa jamii kwa kufuata sera na sheria za nchi zilizopo katika kumlinda mtoto na wanawake dhidi ya ukatili wa kijinsia na kuachana na mila na destuli zilizopitwa na wakati na kumpa uhuru mwanamke kuolewa na mtu anaemtaka.