Na Mwandishi wetu,timesmajira,online
WAWEKEZAJI nchini wameshauriwa kuhakikisha wanazalisha na kuwekeza bidhaa zenye ubora halisi utakaowawezesha watanzania kununua na kutumia bidhaa hizo ziaid ya mara moja badala ya kununua mara kwa mara.
Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzii Mtendaji wa Kampuni ya Nissan Tanzania, Christophe Henning wakati wa uzinduzi wa gari mpya aina ya Nissan Magnite amesema uwepo wa mazingira mazuri nchini Tanzania unawapa nafasi ya kutengeneza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu.
Amesema kutokana na fursa hiyo wanaona ni vema kutangaza gari mpya ambayo inayofanya kununuliwa na watu wa kipato chochote cha chini,kati na juu ambalo linaubora uliokidhi kiwango.
Henning amesema ni wakati wa watanzania kuchangamkia fursa ya gari hiyo kwani ni miongoni mwa magari ambayo linalotumia mafuta kidogo katika safari zake.
“Uletwaji wa gari hili Jipya la nissan Magnite tunaangalia hali ya watanzania hata katika kufanya matengenezo ya gari inakuwa kwa bei nafuu kabisa,” amesema
Kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni hiyo,Alfred Minja amesema hali ya biashara nchini Tanzania kwa kipindi cha miaka miwili iliyumba kutokana na ugonjwa wa Uviko 19 lakini hivi sasa biashara zinaanza kurudi kama kawaida
“Mazingira ya uwekezaji katika serikali ya awamu ya sita yanaonekana kuwa na viashiria vya kuelekea pazuri kwani serikali imeboresha miundombinu yake hususani katika ukusanyaji wa kodi na kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji,” amesema.
Amesema mwelekeo wa biashara na uwekezaji hivi sasa ni mzuri kwani serikali imefungua mianya yote ya ufanyaji biashara na mazingira yameboreshwa.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu