Na mwandishi wetu,Timesmajira
SERIKALI ya mapinduzi Zanzibar imewataka waumini wa dini ya kiislamu kuwa na utamaduni wa kumtanguliza mungu siku zote za maisha yao.
Akizungumza kwenye kongamano la pili la tuzo za Tameya Waziri wa Nchini Ofisi ya mapinduzi Zanzibar, Sada Mkuya ambaye alimuwakilsha Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Mwinyi kwenye kongamano la dini hiyo lililofanyika katika ukumbi wa mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam
“waumini wa dini ya kiislamu jengeni utaratibu wa kusaidiana vipindi vya shida na raha kwa kumtanguliza mungu siku yeyote na nyakati zozote ndani ya maisha yenu ” amesema Mkuya
Aidha waziri Mkuya amesema ya Tameya imekuwa kawaida yake kutoa tuzo mbalimbali za kiteknoloja, mazingira na maarifa kwa waumini wake mbayo ni fursa wezeshi kwa watanzania wa Imani hiyo.

Mkuu wa Taasisi hiyo Shekh Saleh Amer amesema kwamba vijana wanahitaji kuongezewa uwezo dhidi ya ufanisi katika utafutaji wa majukumu mbalimbali ya utendaji kazi
Fursa hizo huacha alama chanya ndani ya jamii ya kitanzania.

Amesema malengo makubwa ya Taasisi hiyo ni pamoja na kuwasaidia wenye uhitaji , uchimbaji wa visima, ujenzi wa misikiti sambamba na kuwapeleka waumini kwenda kuhiji maka na umra
Kwa upande wake mwezeshaji wa Taasisi hiyo Abdaallah Munifu amesema kwa Kundi la vijana ndio lenye kuhitajika kufanya fikra wezeshi ndani ya maisha

More Stories
Mbega ataka viongozi kuimarisha ulinzi kudhibiti wageni
Mbega ataka viongozi kuimarisha ulinzi kudhibiti wageni.
Kero za Walimu kutoshughulikiwa kwa wakati chanzo Cha msongo wa mawazo-CWT