Na Mwandishi Wetu,, Timesmajira Online
KAMPUNI ya Mixx imejivunia kuendelea kuongezeka kwa idadi ya wateja wake pamoja na matumizi ya huduma zake za kifedha kidijitali.
Hiyo imekuja kufuatia mwitikio mkubwa wa Watanzania katika kampeni ya “Kila Muamala ni Bao la Ushindi”, inayofanyika kwa ushirikiano na kampuni ya Hisense.
Akizungumza wakati wa droo ya pili ya kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Biashara wa Mixx, James Sumari, amesema kampeni hiyo imekuwa kichocheo muhimu katika kuhamasisha matumizi ya njia rasmi za malipo ya kidijitali, huku idadi ya watumiaji wa huduma za Mixx ikiendelea kuongezeka nchini.

Sumari amesema moja ya mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi hicho ni kuongezeka kwa matumizi ya Mixx Super App, ambayo watanzania zaidi ya milioni moja wanatumia App hiyo.
Amesema, hatua hiyo inaonesha imani kubwa ya Watanzania katika huduma za kidijitali na mchango wake katika kurahisisha miamala ya kifedha.
Ameeleza kuwa, matumizi ya huduma za kidijitali kama Mixx yanasaidia kuimarisha usalama wa fedha za watumiaji, kupunguza utegemezi wa fedha taslimu na kuwezesha ufuatiliaji wa matumizi ya kifedha kwa urahisi zaidi kwa watu binafsi na wafanyabiashara.
Kwa mujibu wake, huduma hizo pia zinachangia kujenga nidhamu ya matumizi ya fedha, kuongeza uwazi katika shughuli za biashara na kusaidia usimamizi bora wa mapato, jambo linalochochea ukuaji wa uchumi wa kidijitali nchini.

Ameongeza pia, siri ya kushindi ni katika Kampeni hiyo ni kutumia zaidi Mixx Super App, kufanya miamala mingi kidigitali, kutumia huduma za Mixx kama Lipa kwa Simu ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kushinda.
Wakizungumza baada ya kupokea zawadi zao, baadhi ya washindi wa kampeni hiyo wamesema ushindi huo umewapa hamasa zaidi ya kuendelea kutumia huduma za Mixx katika shughuli zao za kila siku.
Mmoja wa washindi hao, Sabdiki Vike, amesema alipokea taarifa za ushindi wake kwa mshangao mkubwa kwani awali alidhani ni utani au jaribio la utapeli.
Hata hivyo, baada ya kuwasiliana na kampuni na kufika katika makao makuu ya Mixx, alithibitisha kuwa alikuwa mshindi halali wa kampeni hiyo.

Amesema matumizi ya Mixx Super App yamemrahisishia kupata huduma mbalimbali za kifedha katika sehemu moja na kufanya miamala kwa haraka na kwa urahisi, jambo ambalo limemfanya kuwa mtumiaji wa mara kwa mara wa huduma hiyo.
Kwa upande wake, Benson Benjamin amesema Mixx imekuwa msaada mkubwa katika kufanya miamala yake kwa usalama na urahisi zaidi.
Ameeleza kuwa, tangu kuanza kwa kampeni hiyo ameongeza matumizi ya huduma za Mixx, hali ambayo anaamini imechangia ushindi wake.
Benjamin ameongeza kuwa anatamani kushinda zawadi kubwa ya safari ya kwenda Mexico kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia, jambo ambalo limemhamasisha kuendelea kutumia huduma za Mixx ili kuongeza nafasi ya kushinda.
Jumla ya washindi 20 walipatikana katika droo hiyo, wakitoka katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Zanzibar, Arusha na maeneo mengine ya nchi.
Mbali na washindi wa fedha taslimu wa shilingi milioni moja moja kila siku, baadhi yao pia walijishindia vifaa mbalimbali vya nyumbani kutoka Hisense, ikiwemo televisheni ya inchi 55, spika na jokofu, baada ya kutumia huduma za Mixx kufanya miamala.
Lengo la pili la Kampeni ya “Kila Muamala ni Bao la Ushindi” inalenga kuhamasisha matumizi ya huduma za kifedha kidijitali huku ikiwazawadia wateja wanaofanya miamala kupitia Mixx. Kampeni hiyo inaendelea kuwa sehemu ya juhudi za kukuza ujumuishaji wa kifedha na kuharakisha matumizi ya teknolojia katika huduma za kifedha nchini.

More Stories
Kampeni ‘Kila muamala bao laushindi’ yazinduliwa Zanzibar
Magu bingwa UMITASHUMTA
Washindi ‘Kila muamala bao la ushindi’ wakabidhiwa zawadi