April 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Watanzania waombwa kuchangia ujenzi bweni la wasichana

Na Penina Malundo,Dar es Salaam

KAIMU Naibu Makamu wa Chuo anaeshughulikia,Taaluma ,Utafiti na Ushauri wa Kitaalam kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe,Dkt.Eliza Mwakasangula amewaomba Watanzania wakiwemo Wanafunzi waliomaliza Chuo hicho Cha Mzumbe miaka ya nyuma kujitokeza na kuchangia Kampeni ya ujenzi wa bweni la wanafunzi wakike mkoani Mbeya.

Akizungumza hayo jana jijini Dar es Salaam
katika Maonesho ya Biashara ya 47 ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ,amesema kwa kufanya hivyo ni ishara ya
kurudisha kitu kidogo kwa jamii ikiwa nao ni wanajamii wa chuo kikuu Mzumbe.

Amesema ujenzi wa bweni hilo ambalo tayari limezinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Homera linahusisha watanzania mbalimbali kwa kutumia namba maalum ya uchangiaji wa Kampen ya Ujenzi wa bweni hilo la Watoto wakike.

“Niwakaribishe wanafunzi waliosoma Mzumbe kurudisha kitu kidogo kwa jamii kuonyesha kuwa ni miongoni mwa wanajamii wa Chuo Kikuu cha Mzumbe,”amesema.

Dkt,Mwakasangula amesema chuo Cha Mzumbe ni miongoni mwa vyuo vinavyotoa Mafunzo mbalimbali ikiwemo masomo ya Biashara,Utawala na Management,Sheria,Uhasibu,Sayansi na Teknolojia ambapo wanateknolojia mbalimbali kwa vijana wao ambao wamekuwa wakizianzisha chuoni hapo.

Amesema hadi sasa chuo kina kampasi tatu Mkoa wa Morogoro,Dar es Salaam maeneo ya Upanga na Tegeta pamoja na Mkoani Mbeya.

“Katika maonesho ya Mwaka huu tunatoa huduma mbalimbali kama kudahili Wanafunzi wapya kwaajili ya kujiunga na programu zetu kwa ngazi ya Shahada za Awali kwa watu waliomaliza miaka iliyopita lakini hata kwa vijana waliomaliza Kidato cha nne na sita tayari dirisha la la udahili tumelifungua,”amesema.

Dkt,Mwakasangula amesema hivyo anatoa wito kwa vijana wanaohitaji kuja kujisajili na Chuo hicho kufika katika Banda lao hili kuweza kujisajili na kuona kazi mbalimbali wanazozifanya.