May 10, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Prof.Muhongo achangia saruji mifuko 280,kuwezesha ujenzi wa zahanati 3

Fresha Kinasa, Timesmajira Online, Musoma

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini Mkoa wa Mara Prof. Sospeter Muhongo amechangia mifuko ya saruji 280 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati tatu jimboni humo.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha Wananchi wa vijiji hivyo wanapata huduma za afya karibu na makazi yao.

Ambapo zahanati ya Kijiji cha Kataryo ametoa mifuko ya saruji 50,zanahati ya Kijiji cha Mabuimerafuru mifuko 50, pamoja na Zahanati ya Kijiji cha Chimati ambapo ameshatoa mifuko 150 huku akiahidi kuongeza mifuko mingine 30.

Hayo yamebainishwa Aprili 27, 2024 kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo hilo.

Taarifa hiyo imesema licha ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Chimati kuanza mwaka 2017 lakini hata msingi bado haujakamilika na Kijiji cha Kaburabura wanakamilisha eneo la ujenzi.

Prof. Muhongo amesema kuwa michango ya inayotolewa na jamii inapaswa kuelekezwa kwenye miradi ya manufaa kwa wananchi wengi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa zahanati na shule.

Pia, amewaomba wananchi na wadau wa maendeleo jimboni humo walioahidi michango yao ya kufanikisha miradi ya maendeleo watoe kuepusha malalamiko.

Kwa upande wake Juma Maira Mkazi wa Kijiji cha Kataryo amesema anamshukuru Mbunge wa Jimbo hilo kwa kuendelea kuchangia miradi ya Kijamii ambayo inagusa moja kwa moja maisha ya wananchi.