Na Esther Macha, Mbeya
HOSPITALI ya Rufaa Kanda ya Mbeya imetoa elimu ya kupambana maambukizi ya virusi vya Corona kwa watu wenye ulemavu wa kusikia .
Akizungumza na majira juzi ofisini kwake Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya, Dkt .Godlove Mbwanji alisema mbali ya kutoa elimu kundi hilo pia wameweza kutoa kutoa elimu kwa wafanyakazi wa hospitali.
Dkt. Mbwanji alisema kwamba wameona ni muhimu kutoa elimu kwa kundi hilo kutokana na hali halisi ya mazingira ya watu wenye ulemavu wa kusikia ilivyo.
“Ni muda mwafaka kusaidia kundi hili ili lisiweze kuangamia na gonjwa hili hatari ,tumejitahidi kuwakusanya kwa pamoja na kuwapa elimu hii muhimu kwao ili waweze kujikinga”alisema Mkurugenzi huyo.
Aidha Dkt. Mbwanji alisema kuwa mbali ya kutoa mafunzo hayo hospitali imechukua tahadhari nyingine ikiwa ni pamoja na kupunguza msongamano wodini kwa kuruhusu watu wachache kuingia wodini kuona wagonjwa.
Alisema kuwa kwa kuanzia walianza kutoa elimu kwa ndugu wa wagonjwa katika kupunguza idadi ya ndugu ambao wanakuja kuona wagonjwa ambao wataingia ndugu wawili kila wakati kwa kupeana nafasi ya kuingia kwa kadi maalum pamoja na kunawia dawa ya vitakasa mikono.
Hata hivyo Dkt. Mbwanji alisema hivi sasa kila mmoja amechukua tahadhari ya kupambana na ugonjwa huu kwa kunawa mikono pia kuweka vitakasa mikono maeneo ya ofisi na biashara yakiwemo masoko.
More Stories
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi
Rais Samia apongezwa kwa kuboresha huduma kwa wazee
Madaktari bingwa wa Samia watua Rukwa