April 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wasabato waja na muarobaini wa kutengeneza kizazi chenye maadili

Na Hadija Bagasha, TimesMajira Online, Tanga

VIONGOZI wa kiimani wametakiwa kutumia programu zao za maadili kwenye majukwaa ya makanisa yao kufundisha maadili hususani katika kipindi hiki ambacho kuna wimbi la watotot weanaojiunga na vikundi vya kiasi.

kauli hiyo imetolewa wakati jeshi la polisi Mkoani Tanga likiwa linaendelwa na operesheni ya kukabiliana na vikundi vya watoto vinavyojiita watoto wa ibilisi.

Juliasi Mbwambo ni mchungaji wa kanisa la waadiventista wasabato Kana jijini Tanga ,anaona umuhumu wa majukwaa ya kiimani kutumika kuwafundisha maadili mema vijana wenye umri mdogo.

Viongozi wa watoto wa kanisa la waadiventista wasabato Kana anasema programu za watoto zinatakiwa kupewa kipaumbele kutengeneza kizazi cha jamii yenye hofu ya Mungu.

“Pamoja na kuwafundisha watoto makanisani tunategemea wanapofika shuleni wakawe mabalozi kwa wenzao hivyo tunategemea jamii kubwa ya watoto itabadilika kutokana na Programu hizi”alisema Lyimo.

Watoto wanaona umuhu wa wao kuingizwa kwenye ratiba za mara kwa mara wakati wa ibada na masaa ya ziada ,wakiamini programu hizo zitawakuza kwenye njia inayompendeza mungu.

Mpango huo wa kuwatengeneza kimaadili vijana unatumainiwa huenda ukaleta mabadiliko chanya ya kitabia ndani ya jamii na hivyo kuwa na kizazi chenye kumuogopa Mungu wakati wote wa maisha yao.

Programu hizo za watoto wa umri wa miaka 4-9 kwa makanisa ya waadventista wasabato dunia zimekuwa zikifanyika kila Mwaka katika kanisa hilo la waadventita Duniani kote