May 8, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

‘Wanawake Mkoa wa Kilimanjaro wanaongoza kwa uzito uliopitiliza’

Na Martha Fatael,TimesMajira Online,Moshi

SERIKALI imesema pamoja na Mkoa wa Kilimanjaro kufanya vizuri kwa kiwango kidogo Cha udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano lakini wanawake wa mkoa huo wanaongoza kwa uzito uliopitiliza.

Pamoja na Mkoa wa Kilimanjaro wenye asilimia 20,lakini pia mkoa wa Dar es Salaam unafuatia kwa kuwa na kiwango cha udumavu kwa asilimia 20.1.

Waziri wa Kilimo Prof Adolph Mkenda amesema hayo wakati anafunga maadhimisho ya kitaifa ya siku ya chakula Duniani yaliyofanyika Manispaa ya Moshi.

Katikati waziri wa kilimo, Prof Adolf Mkenda, wa kwanza kulia(mwenye miwani) ni mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai wakisikikiza maelezo kwa wajasiriamali walioahiriki maonyesho ya siku ya chakula Dunia iliyofanyika kitaifa mkoani Kilimanjaro.

Aidha Waziri Mkenda amesema mikoa ya Njombe, Iringa na Ruvuma inahali mbaya ambapo Ina kiwango Cha udumavu kwa zaidi ya asilimia 40 na kupita kiwango Cha Taifa Cha udumavu ambacho ni asilimia 31.8.

“Kilimanjaro na Dar es Salaam inafanya vizuri katika suala la lishe bora kwa watoto Chini ya miaka mitano, pamoja na Hilo wakinamama wwnaongoza kwa viriba tumbo” amesema.

Kuhusu Hali ya chakula nchini, Pro.Mkenda amesema hali ya chakula nchini kwa mwaka 2021/22 ni nzuri ambapo Taifa Lina ziada ya zaidi ya Tani Mil 1.9 ikilinganishwa na mwaka ulipopita 2020/2021.

Amesema kwa mwaka huu Serikali ina Tani Mil.18.42 za mazao ya Nafaka na zisizo za nafaka ikilinganishwa na mwaka ulipopita ambapo uzalishaji ulikuwa Tani Mil 18.19.

Amesema katika mipango ya Serikali ya kuboresha zaidi sekta ya Kilimo, serikali imeongeza bajeti ya utafiti wa mbegu na Kilimo bora kutoka Sh Bil 7 hadi Sh Bil 11.63 mwaka 2021/2022.

Waziri Mkenda amesema pia serikali imeongeza bajeti ya huduma za Ugani kutoka Mil 603 hadi Sh Bil 11.5 mwaka 2021/2022.

Awali mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Steven Kagaigai amewataka wananchi kuzingatia utunzaji wa chakula lakini pia kuuza ndani na nje ya nchi kwa miongozo ya serikali.