
Na Israel Mwaisaka,Nkasi
JAMII imetakiwa kujiunga na bima ya afya katika utekelezaji wa mpango wa bima ya afya kwa wote ili kuwa na uhakika wa matibabu pale wanapougua.
Wito huo umetolewa jana na mkuu wa wilaya Nkasi mkoani Rukwa Mohamed Mtulyakwaku kwenye mkutano wa hadhara katika mji wa Namanyere ambapo alidai kuwa bima ya afya ni muhimu sana na ndiyo maana serikali ilikuja na mpango huo.
Alisema kuwa ni jukumu la kila mmoja kuhamikisha anajiunga na mfuko wa bima ya afya kwani tunaelekea katika wakati ambapo kila anayehitaji matibabu hataweza kupata huduma hiyo hadi pale atakapokuwa amejiunga katika bima.
hivyo aliwataka viongozi kuanzia ngazi ya vitongoji na kuendelea kuhakikisha wanatoa elimu na kuwahamasisha Wananchi kujiunga na bima ya afya kwani nchi kwa sasa huo ndiyo mwelekeo wake na mafanikio ya mpango huo yatatokana na uelewa watakaoupata kutoka kwa viongozi wao.
sambamba na hilo ameitaka jamii kuchukua hatua juu ya mvua za El-Nino kwa kuhakikisha wanachukua tahadhari ya kutosha ili kuweza kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na mvua hizo.
alifafanua kuwa mamlaka ya hari ya hewa Nchini (TMA) ilishatoa tahadhari juu ya kuwepo kwa mvua hizo ikiwa ni pamoja na hatua za kuchukua katika wakati wote wa mvua hizo na kuwa ni muhimu hatua zote za tahadhari ya mvua hizo kufuata ili kuondokana na madhara yanayoweza kutokana na mvua hizo.
mkuu huyo wa wilaya pia aliutumia mkutano huo kusikiliza kero mbalimbali za Wananchi ambapo nyingi zilitatuliwa papo hapo huku akiwtaka viongozi kutozoea matatizo ya Wananchi kwa kuchukua hatua haraka pale utatuzi ya kero yoyote ya mwananchi inapojitokeza.
huo ni mkutano wake wa kwanza wa kuzungumza na Wananchi na ikiwa kama ni sehemu ya kujitambulisha kwa Wananchi tangu ahamie katika wilaya Nkasi

More Stories
Dkt.Mabula ataka kasi mpya maendeleo Tabora
Rais Samia apiga kura Chamwino,kumpata Mrithi wa Ndejembi
Serikali yaendelea kupunguza makali ya bei za mafuta