March 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Meneja wa PSSSF Mkoa wa Temeke, James Mlowe, akibadilishana mawazo na Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF, Abdul Njaidi (kulia) na Afisa Uhusiano wa Mfuko huo, Meseka Kadala

Wanachama watakiwa kufika PSSSF kuhakiki taarifa zao

Na Mwandishi Wetu, Sabasaba.

WANACHAMA wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wametakiwa kufika kwenye ofisi za Mfuko huo zilizoenea katika mikoa yote nchini ili kuhakiki taarifa zao.

Meneja wa PSSSF mkoa wa Temeke, James Mlowe (kulia), akimuhudumia mwanachama wa Mfuko aliyefika kwenye banda la PSSSF viwanja vya Julius Nyerere

Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa maonesho ya 44 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam kwenye banda namba 13 la Mfuko huo kwenye viwanja vya Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Julai 3, 2020, Meneja wa PSSSF Mkoa wa Temeke, James Mlowe amesema mwanachama akifika kwenye ofisi yoyote ya PSSSF utaratibu na mahitaji yako vile vile hivyo amewahimiza kufanya hivyo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kutokana na kutohakiki taarifa.

Afisa wa huduma kwa wateja mwandamizi wa PSSSF, Nelusigwa Mwalugaja (kushoto), akimfafanulia mwanachama huyu kuhusu michango yake.

Lakini pia amewaalika wanachama watakaotembelea kwenye viwanja vya Julius Nyerere kwenye maonesho hayo ya biashara maarufu kama sabasaba, wataweza kujipatia huduma zote kama zinavyotolewa kwenye ofisi za Mfuko kwenye mikoa yote nchini.

Afisa Mafao PSSSF, Abddallah Juma Adam (kulia), akitoa huduma kwa mwanachama aliyetembelea banda namba 13 la Mfuko huo kwenye Viwanja vya Julias Nyerere maarufu Sabasaba.

“Tulichofanya mwaka huu tumehamisha miundombinu na vifaa vyote vya kutoa huduma vinavyopatikana kwenye ofisi zetu ikiwemo makao makuu, hivyo mwanachama anapofika kwenye banda letu anapata huduma zote ikiwemo, taarifa za michango, mafao, pensheni na mafao yanayotolewa na Mfuko” amefafanua Mlowe. 

Maonesho hayo yaliyoanza Julai 1, 2020 yamefunguliwa rasmi Ijumaa Julai 3, 2020 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na kauli mbiu ya mwaka huu ni “Uchumi wa viwanda, ajira na biashara endelevu”.

Mwanasheria wa PSSSF, David Mnkande (kulia), akifafanua kuhusu huduma za kisheria za Mfuko huo kwa wanachama hawa waliotembelea banda la PSSSF.
Afisa Matakelezo Mwandamizi wa PSSSF, Donald Meeda (kushoto), akimfafanulia masuala mbalimbali ya huduma za Mfuko, mwanachama huyo aliyepata fursa ya kutembelea banda la PSSSF.
Afisa Matekelezo PSSSF, Zainab Ndullah (kushoto), akimuhudumia mwanachama wa Mfuko huo.