May 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wamiliki wa fremu za biashara watakiwa kulipa kodi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Wamiliki wa fremu na majengo ya biashara mkoani Arusha wametakiwa kulipa kodi ya zuio ya asilimia 10 badala ya kuliacha jukumu hilo mikononi mwa wapangaji jambo ambalo limetajwa kukwamisha ustawi wa biashara zao kwa kuwafanya walipe kodi mara mbili.

Awali akizungumza wakati akitoa ripoti ya mwenendo wa kampeni ya elimu ya kodi ya Mlango kwa Mlango inayoendeshwa na maafisa wa mamlaka hiyo,Meneja wa TRA Mkoa wa Arusha Eva Raphael anabainisha kero inayokumba wafanyabiashara ikiwemo wamiliki wa nyumba kukwepa kodi hiyo na kulazimisha wapangaji kulipa jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Kufuatia changamoto hiyo mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela anatoa maelekezo kwa wafanyabiashara ikiwemo wamiliki wa majengo kulipa kodi kwa mujibu wa sheria, ili kuunga mkono Serikali katika sekta mbalimbali za kimaendeleo.

Nao baadhi ya wafanyabiashara waliofikiwa na Kampeni hiyo wameishukuru mamlaka ya mapato kwa kutoa elimu kwa wafanyabiashara pamoja na kusikiliza kero mbalimbali zinazo wakabili.

Afisa Msimamizi wa kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Jamal Ngarawa akitoa Elimu ya kodi kwa Bw. Michael Mshana, mfanyabiashara wa Arusha mjini ikiwa nikatika zoezi maalumu la Elimu ya mlango kwa mlango yeye lengo la kuwafikia wafanyabiashara wa mkoa Arusha kuwapa elimu ya kodi na kusikilza changamoto na malalamiko mbali mbali ya kodi kwa lengo la kuyatatua.