Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online- Dar
WAFANYABIASHARA wilayani Ilala wametakiwa kushiriki kampeni ya Serikali ya usafi kwa ajili ya kulifanya Jiji la Dar-es-Salaam liwe na madhari ya kupendeza na kuvutia.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo,amezungumza Julai 25,2026 wakati wa kampeni endelevu ya usafi wa mwisho wa mwezi ambao imewashirikisha watumishi wa halmashauri hiyo pamoja na kampuni za usafi ikiwemo SATEK na JUZA.

Ambapo amewataka wafanyabiashara waliopo wilayani Ilala kushirikiana na Serikali kuhamasisha kampeni hiyo ya usafi katika maeneo yao ya biashara kila wakati hususani kila jumamosi.
Huku akizitaka na kampuni za usafi kuhakikisha wana timiza wajibu wao kwa kuondoa taka kwa wakati ili kuepuka mrundikano wa taka mbele ya maduka na biashara.
Amesema uwekezaji unaofanywa na Serikali katika sekta ya afya hautakuwa na tija ikiwa wananchi hawatazingatia usafi wa mazingira wanayoishi pamoja na yale wanayofanyia kazi.
“Afya bora huanzia kwenye kinga huku usafi ukiwa nguzo muhimu ya kujikinga dhidi ya magonjwa.Nawashukuru Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kwa kujitolea kwenu,naomba mitaa yote iliopo Ilala iwe safi kwa kuendeleza kampeni hii ya usafi ya Serikali kwa kufanya usafi kila siku na kushiriki usafi wa mwisho wa mwezi pamoja na wananchi,”amesema Mpogolo.




More Stories
Wakala wa Vipimo washiriki NBC Marathon Dodoma
Miundombinu ya shule yatakiwa kulindwa
Waziri Kikwete akutana na viongozi Chalinze wajadili Dira 2050