April 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waandishi wa habari wanawake watoa msaada kwa watoto wenye ulemavu


Na Esther Macha,TimesMajira, Online,Rungwe
WATOTO wenye ulemavu katika shule ya msingiĀ  mchanyiko ya Katumba (2)iliyopo wilayani Rungwe MkoaniĀ  Mbeya wamepatiwa msaada wa vitu mbali mbali shuleni hapo ikiwa ni sehemu ya kuwafariji watoto hao kutokana na hali walinazo.
Msaada huo ulikabidhiwa na waandishi wa habari wanawake wa mkoa wa Mbeya waliotembelea shule hiyo kwa lengo la kuwafariji watoto hao ambao wanatoka mikoa mbali mbali hapa nchini .
Akipokea Msaada huo kwa waandishi wa habari wanawakeĀ  Mkuu wa shule ya msingi Mchanganyiko ya Katumba (2) MauyeniĀ  Kilumbe amesema kwamba kitendo cha kufika tu kuwaona watoto hao ni faraja kwani huona kama jamii imewatenga na kuwaona tofauti.
Vitu vilivyokabidhiwa ni pamoja na Sabuni ,Juice , Soda , Mafuta ya kupakaa ,Pipi , pamoja na Pedi kwa watoto wa kike .
Aidha Kilumbe aliwatoa hofu wazazi kuona hawa watoto wana haki ya kupata elimu hivyo wanapaswa kuwapenda wasione kwamba ulemavu wao hawana budi ya kusoma.
ā€œNdugu zangu nyie waandishi wa habari mnatembea sana muwe mnajaribu kutoa elimu kwa wazazi maana nyie mnapita maeneo mengi,mnaweza kutusaidia sana kuna watoto wengi wapo majumbani wamefichwa ā€œamesema Mkuu huyo wa shule.
Akizungumzia kuhusu idadi ya watoto walemavu waliopo shuleni hapoĀ  mkuu huyo wa shule amesema kwamba mpaka sasaĀ  wana walemavu 277 wa aina tano na kusema karibu wote wanakaa shule huku akidai kuwa ni walemavu wachache wanaotoka jirani na katumba ambao hawakai shule.
Akielezea zaidi Kilumbe amesema kuwa kwa mwaka huu wamepokea watoto wenye ulemavu 58 kutoka mikoa mbali mbali na kudai kuwa wana idadi kuwa ya watoto wenye ulemavu wa akili ambayo ni 138Ā  ukilinganisha na ulemavu mwingine.
Kwa upande Sifa Robert ambaye ni mzazi ambaye amefika kumuona mtoto wake mlemavu alisema kwamba anaona fahari kumuona mtoto wake licha ya kuwa na ulemavu na kuwashauri wazazi na walezi wenye watoto kuwapeleka shule watotoĀ  na si kuwafungia ndani kama ilivyojengeka kwa baadhi ya wazazi wengine.
ā€œNawaasa wazazi na walezi kuwa na moyo wa upendo kwa watoto hawa kwani makusudi ya mwenyezi Mungu hivyo hawapaswaswi kuwachukiaĀ  au kuwatenga watoto ,nimeona baadhi ya familia zingine hutenga chumba maalum kwa watoto wenye ulemavu na kutenga chakula cha peke yaoĀ  hii si sawa wazazi tunafanya vibaya tubadilike tunapofanya hivi hatuwatendei haki watoto hawa ā€œalisema Sifa.
Mmoja wa waandishi wa habari wanawake, Mary Mwakibete amesema kuwa watoto wenye ulemavu wanahitaji faraja hata usipochukua chochote bado ni faraja kubwa sana .
Aidha Mary ameomba wadau mbali mbali kujitokeza kusaidia shule hiyo yenye changamoto ya uzio ambapo hufanya watoto wenye ulemavu wa akili kutoroka kitu ambacho ni hatari .