April 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

UVIKO-19 yadhoofisha uchumi Kenya

NAIROBI, Ukuaji wa uchumi nchini Kenya umeshuka kwa kiwango cha asilimia 0.3 mwaka 2020 kutokana na athari za janga la virusi vya Korona (UVIKO-19), licha ya uchumi hup kukuwa kwa asilimia tano mwaka 2019.

Waziri wa Fedha, Ukur Yattani kupitia takwimu alizozitoa, kiwango cha mfumuko wa bei kilipanda kutoka asilimia 5.3 mwaka 2019 hadi asilimia 5.4 mwaka 2020 kutokana na mikakati ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Korona, iliyodumaza usambazaji wa bidhaa.

Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2021 zinazoangazia mwaka 2020 kuhusu maendeleo ya uchumi Kenya, pato la taifa kutoka sekta ya utalii limepungua kwa asilimia 43.9 hadi shilingi bilioni 91.7 mwaka 2020 huku idadi ya wageni kwenye hoteli ikipungua kwa asilimia 58.0 mwaka huo hadi watu milioni 3.8.

Idadi ya wageni waliowasili Kenya mwaka 2020 ilipungua kwa asilimia 71.5 hadi 579,600 ikilinganishwa na mwaka 2019.

Aidha, kiwango cha biashara kilipungua hadi shilingi trilioni 2.29 huku thamani ya bidhaa zilizoingizwa Kenya ikiwa ni shilingi trilioni 1.64 wakati thamani ya bidhaa zilizosafirishwa nje ya nchi ikiwa ni shilingi trilioni 0.64.

Wakati huo huo, kwa usafiri wa ndege, idadi ya wasafiri ilipungua kwa asilimia 62.5 kutoka watu milioni 12.0 waliosafiri Kenya mwaka 2019 hadi watu milioni 4.5 mwaka 2020 wakati kiwango cha mizigo kikipungua kwa asilimia 8.9

Kwa mujibu wa Waziri huyo, kiwango cha mfumuko wa bei za bidhaa kilipanda kutoka asilimia 5.3 mwaka 2019 hadi asilimia 5.4 mwaka 2020 kutokana na mikakati ya serikali ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Korona.

Hali iliyolemaza usambazaji wa bidhaa na kuongeza bei za bidhaa hasa katika sekta ya uchukuzi na nishati, serikali inatarajia kiwango hicho kitaongezeka hadi mwishoni mwa mwaka 2021.