May 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

UTEUZI : Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo kuongoza PSSSF, aliyekuwa PSSSF kupangiwa kazi nyingine

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi kama ifuatavyo:

  1. Amemteua Dkt. Thomas Nestory Bwana kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI).

 Kabla ya uteuzi huu Dkt. Bwana alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Mazingira (Biodiversity Conservation) Ofisi ya Makamu wa Rais. Anachukua nafasi ya Dkt. Geofrey Mkamilo ambaye amemaliza muda wake.

Uteuzi huu umeanza tarehe 03 Februari, 2024.

  • Amemteua Abdul-Razaq Badru kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).

Kabla ya uteuzi huu Bw. Badru alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu (HESLB). Aidha aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA Hosea Kashimba atapangiwa kazi nyingine.

  • Amemteua Dkt. Bill Kiwia kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).
  • Dkt. Kiwia anachukua nafasi ya Bw. Badru ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).

Uteuzi huu unaanza tarehe 06 Februari, 2024

Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu