Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online- Mwanza
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limeimarisha hali ya usalama na wananchi wanaendelea na shughuli zao za maendeleo.
Kupitia taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Wilbrod Mutafungwa, aliyoitoa leo Julai 07.2026,amesema jeshi hilo limeimarisha hali ya usalama kwa kuwapanga askari katika maeneo muhimu kwa lengo la kulinda watu na mali zao katika kusherekea sikukuu ya Wafanyabiashara(Sabasaba).

Hivyo amewatoa hofu wananchi huku akisisitiza kuwa ni wajibu wa Jeshi la Polisi kulinda usalama wao.
“Msiogope kuona ongezeko la askari mitaani,bali furahini kwa sababu uwepo huo ndio unaohakikisha usalama wa maisha na mali zenu,”amesema DCP.Mutafungwa.
Huku akionya watu wenye nia ya kusababisha uvunjifu wa amani kuacha mara moja, kwani jeshi hilo limejipanga imara na yeyote atakayejaribu atadhibitiwa kwa mujibu wa sheria.
“Kwa kweli hatutaruhusu mtu yeyote afanye vitendo vya uvunjifu wa amani, atadhibitiwa kisheria na kwa nguvu kubwa,”amesema DCP.Mutafungwa.
Pia,amesema Jeshi la Polisi linaendelea kuimarisha usalama na kufuatilia kwa karibu taarifa za wahalifu zinazotolewa na wananchi wema.




More Stories
Mhitimu asiyeona aeleza mafanikio ya useremala VETA
JNHPP: Ndoto ya Nyerere yatimia,Rais Samia apongezwa
Rais Samia aagiza wakuu wa Mikoa kujiandaa na udhibiti wa Athari za El Nino