December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Urio ashukuru kuteuliwa kwa mara nyingine

Na Mwandishi wetu,TimesMajira,Online

MGOMBEA Udiwani Kata ya Kunduchi kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM),Michael Urio amerudisha fomu huku akiwashukuru Viongozi wa Chama cha Mapinduzi kwa kumuamini kwa mara nyingine.

Akiwa ameongozana na Wanachama wa Chama hicho wakati akirudisha fomu hiyo,amewashukuru na kuwaomba ushirikiano katika kuhakikisha wanapeperusha vema bendera ya Chama hicho.

Urio amesema kuwa kwa kushirikiana na chama chake atahakikisha anasimamia kikamilifu amani na mshikamano katika kipindi chote cha kampeni.