December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

‘Unyonyeshaji lishe bora ya udumavu’

Na Severin Blasio,Morogoro

WITO umetolewa kuwa wanaojifungua wameshauriwa kunyonyesha watoto wao ipasavyo ili kuboresha ukuaji na hali ya lishe ya mtoto.

Ushauri huo umetolewa mjini Morogoro na Ofisa Afya wa Manispaa hiyo Ester Kawishe,wakati mafunzo ya lishe kwa wanahabari Mkoa wa Morogoro ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya unyonyeshaji duniani.

Aidha Kawishe amesema mtoto akinyonya ipasavyo kutapunguza uwezekano wa kupunguza magonjwa sugu kama vile kisukari,magonjwa ya moyo,pumu na baadhi ya saratani kwa akina mama na hata udumavu.

Pia mwanamke akinyonesha ipasavyo kunapunguza uwezekano wa kuwa na uzito uliozidi au kiribatumbo na ikiwa ni pamoja na kupungua vifo vya watoto vinavyosababishwa na upungufu kingamwili ya mtoto.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni ‘Tuwawezeshe wanawake kunyonyesha kwa afya bora na ulinzi wa mazingira’.

Awali akifungua mafunzo hayo Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro Dkt.Kasirye amewaasa wanahabari kuhakikisha wanafikisha ujumbe kwa jamii kuhusu dhana nzima ya unyonyeshaji kwa siku 1000 za makuzi ya mtoto.

“Ofisi yangu itaendelea kutafuta namna mbalimbali za kuwajengea uwezo wanahabari katika masuala mbalimbali yanayohusu afya.