May 16, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Unguja waadhimisha siku ya kuzaliwa Rais Samia pamoja na kupanda miti

Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline,Dodoma

MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, Leo Jumamosi Januari 27 2024, ameungana na Viongozi wengine wa Kitaifa pamoja Wananchi mbali mbali, katika Zoezi la Upandaji Miti, huko Donge Muwanda, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Zoezi hilo ambalo ni Sehemu ya Mpango wa kupambana na Mabadiliko ya tabianchi, limekwenda sambamba na Kumbukizi ya Siku ya Kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye pia mwenyewe ameshiriki akiwa Mgeni Rasmi.

Viongozi wengine ambao wamejumuika katika Zoezi hilo lililobeba Jina la ’27 YA KIJANI’ ni pamoja na Mawaziri wa Serikali zote Mbili; Viongozi wa Jamii, Dini na Siasa, Watendaji mbali mbali, Wanamazingira, kutoka Ndani na Nje ya Nchi; na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, wote wakiongozwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi,Mhandisi Zena Ahmed Said.