May 8, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Sekta ya chumvi yakabiliwa na changamoto ya ubora

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Ruangwa

MOJA ya changamoto inayoikabili sekta ya chumvi nchini ni ubora wa chumvi,masoko,mitaji na upatikanaji wa vifaa vinavyohusika katika uzalishaji wa bidhaa hiyo .

Hayo yamesemwa na Meneja Uwezeshaji,Uchimbaji mdogo wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Tuna Bandoma wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya Madini yanayoendelea katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

Bandoma amesema kuwa chumvi imekuwa ni kilio kikubwa na serikali imekuwa na mikakati mingi ambapo mojawapo ya mkakati wa serikali ni kukaa na wadau ili kujadili kwa kina changamoto zilizopo pamoja na kujua kwa pamoja suluhu mbalimbali ambazo zinazotokana na sekta hiyo.

“Pia Serikali imekuwa ikichukua hatua na mikakati mbalimbali ikiwemo kuanzisha shamba darasa ambalo wanaenda kuanzisha katika wilaya ya Kilwa,lakini pia inaenda kuanzisha  kiwanda cha kuchakata  chumvi lengo likiwa ni kuongeza ubora ili wazalishaji wa bidhaa hiyo ili iweze kukidhi mahitaji ya soko,

“Na kwa namna hiyo sasa tutakuwa tumewafungulia wazalishaji wa chumvi kupaki chumvi yao kama inavyohitajika kwenye soko na tuna matumaini kwamba kiwanda hicho kitaweza kufungua Zaidi vifungo ambavyo vimekuwepo kwa wazalishaji wa chumvi nchini za kuweza kufikia soko.”amesema na kuongheza kuwa
“Kwa mfano leo hii tuna kongamano ambalo linajadili sekta ya uzalishaji chumvi ambalo litatoa mwanya mwanya kwa wadau kuona sekta zinazoikabili sekta hiyo ili kuja na suluhisho Viwanda vinavyozalisha chumvi vimealikwa ili waje watoe ubora unaotakiwa kwa ajili ya wachimbaji wadogo ambao wamezalisha chumvi kwa kiwango duni ili waweze kujifunza namna ya kuzalisha chumvi yenye ubora”amesema Bandoma

“Kwa hiyo leo hii katika maonyesho haya Pamoja na kushiriki kama taasisi lakini pia  tunayo migodi mbalimbali Pamoja na miradi ya utafiti inayofanyika hivi sasa jambo kubwa zaidi ambalo linaongeza manufaa kwa nchi ni ile kuwalea wachimbaji wadogo kuwajengea uwezo na mfumo kupata mitaji kutoka taasisi za fedha,kupata vifaa vya uchimbaji” ameongeza

Aidha Bandoma ameongeza kuww wai kama STAMICO ukilinganishwa na mashirika mengine ya Serikali ikiwemo shirika la Maendeleo ya Uchimbaji la Zimbabwe ZMDC muundo wake lenyewe linashughulika na maendeleo ya almasi,shirika la Madini Zambia ZIMCO  wao wanajikita Zaidi kwenye uvunaji wa kopa lakini muundo wa shirika la madini la STAMICO kipekee umeakisi manufaa makubwa mawili ikiwa ni Pamoja na shirika kushiriki kama taasisi kwa niaba ya serikali katika kuwekeza katika rasimali ya madini ambayo ni moja ya rasilimali zinazoondosha na pili jukumu lake kubwa kuwajengea uwezo watanzania ili waweze kushiriki,na kupitia kuwajengea uwezo ambapo shirika lao limepewa nafasi ya kuwa mlezi wa wachimbaji wadogo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wazalishaji Chumvi Taifa (FEMATA) Abdallah Ally Ismail amesema wmepokea kwa furaha suala la kuletewa kiwanda cha kuchakata chumvi huku akiiomba Serikali kutimiza ahadi hiyo.

Aidha amesema wamekuwa na changamoto kubwa ikiwemo kuwepo kwa mwekezaji wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani ambaye amekuwa akinunua tani moja kw ash.170,000 kwa maana ya kilo moja ni sh.170 wakati bei ya sokoni ya chumvi kwa kilo ni sh.1000.

“Kwa hiyo tunaomba serikali ituletee kiwanda hicho haraka iwezekanavyo ili tujikwamue na changamoto ya ukosefu wa soko .”amesema

Mwenyekiti huyo amesema kiwanda hicho kitasaidia kuboresha chumvi yenye ubora ambayo itakuwa na ushindani katika soko tofauti na hivi sasa ambapo wamekuwa wakizalisha chumvi ambayo haina ubora na hivyo kukosa soko.

“Tunashukuru kwa kiwanda hiki ambacho tunaamini kitakuja haraka iwezekanvyo nasi tunatoa ahadi ya kuonhggeza uzalishaji wa chumvi yenye ubora lakini pia kulipa kodi kadri ya mapato yatakavyopatikana.”amesema Ismail