May 18, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frédéric Clavier akiongea katika hafla ya kuwapongeza wajasiriamali mbalimbali

Ubalozi wa Ufaransa Tanzania washindanisha wajasiriamali 1,000

Na David John,TimesMajira,Online

SERIKALI  ya Ufaransa kupitia ubalozi wake nchini Tanzania imewashindanisha wajasiriamali 1,000 kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika ikiwemo Tanzania.

Ambapo washindi wa shindano hilo la wajasiriamali  wamepata zawadi mbalimbali hii ikiwa ni kuwatia moyo katika shughuli zao za kijasiriamali.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi  kwa wajasiriamali hao,Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Frédéric Clavier amesema  vyombo vya umma na binafsi kuendelea kushirikiana kwa pamoja  ili kufanikisha malengo makuu yaliyoorodheshwa katika mpango mkakati wa “Tanzania 2025”.

“Ni bahati yangu kuwakaribisha  kwenye  sherehe ya kuwapongeza washindi wa shindano la Wajasiriamali 1000 ambayo Ufaransa tumeandaa, hafla yetu ya “kiuchumi na biashara” iliyowekwa katika Mkutano wa “2020 Africa France Mkutano,”amesema na kuongeza kuwa

“Naomba kusisitiza kiwango cha ushirikiano kati ya Afrika na Ufaransa na kati ya Ufaransa na Tanzania tutaendelea kukiimarisha,”amesema

Ameongeza kuwa sekta ya umma ikiwa ipo mstari wa mbele kuleta uchumi kwa kutekeleza miradi mikubwa ya miundombinu ni vizuri sekta binafsi nayo ipate nafasi ya kushiriki kikamilifu katika  ukuaji wa uchumi wa nchi na kupendekeza ubunifu na suluhisho endelevu.