May 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TUICO yatoa msaada,kusherekea siku ya Wanawake Duniani

Na Penina Malundo, timesmajira

CHAMA cha Wafanyakazi wa Viwanda,Biashara,Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO), Idala ya Wanawake, Afya na Usalama na Watu wenye ulemavu imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa Kituo cha kulelea watoto yatima Cha Dunia heri kilichopo Kimbiji Kigamboni.

Miongoni wa msaada waliotoa ni pamoja na Mchele, Unga, Sukari, Maji, sabuni , chumvi na vitu vingine mbalimbali.

Akikabidhi msaada huo mwishooo mwa wiki Mkuu wa Idara hiyo , Witness Mwijage amesema kuwa wanawake ndio nguzo imara katika familia na jamii hivyo hawanabudi ya kuwasaidia na kujitoa kwa watu  wengine hususani kwa Makundi  ya watu wenye uhitaji.

Amesema Watumishi wanawake kutoka Chama hicho wameugana na  wanawake wengine duniani kote katika kuadhimisha siku hiyo kwa kusherekea na watoto yatima.

Amesema wanawake hao wameamua kutoa  msaada wa vitu mbalimbali katika kituo hicho ikiwa ni Moja ya kusherekea siku hiyo na watoto hao wa Kituo cha kupeleka watoto Yatima.

“Katika kuadhimisha siku ya wanawake  tumeguswa sisi kama wanawake kuja kusherekea siku hii na watoto wa Kituo hiki Cha Dunia heri hivyo tumeguswa kutoa matendo ya huduma Kwa watoto wanaoishi katika kituo hiki,”amesema na kuongeza 

“Tumeguswa kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika kituo hiki  kwetu sisi haya ni matendo ya huruma ukizingatia kipindi hiki ni cha Kwaresma kwa wakristo na ramadhani inakuja kwa waislamu,”alisema.

Aidha ameiushukuru Uongozi  wa TUICO pamoja na wadau wengine ambao wameweza kuwaunga mkono na hatimaye kufanikisha wanawake hao kuwafikia  watoto wa Kituo hicho.

Ametoa wito kwa wanawake wengine kuinga mfano wa Wanawake hao wa kuwa na utaratibu wa kutoa  matendo ya huduma Kwa watu mbalimbali wasiojiweza.

“Nitoe wito kwa wanawake wengine kuwa na utaratibu wa kuwatembelea watu wenye mahitaji maalumu kwa kukaa nao na kuwapa faraja ili nao wajione kama watu wengine na wasisubiri mpaka siku ya wanawake duniani “amesema

Kwa upande wake  Msimamizi wa kituo Cha Dunia heri Beata Kusel ameushukuru uongozi wa  wanawake wa TUICO kwa kuwapatia vitu mbalimbali jambo ambalo limewapa faraja.

Aidha amesema kituo hicho kinawatoto 37 huku watoto 15 wakiwa ni wanafunzi huku wakitarajia kupokea watoto wengine Saba kutoka kijijini.

Awali siku ya wanawake ilitambulishwa rasmi na Umoja wa Dunia mnamo 1977 baada ya kuibuka kwa mara ya kwanza kutoka katika shughuli za utekelezaji wa Karne ya 20 huko Amerika Kaskazini na Ulaya.