May 17, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Malezi, makuzi na maendeleo ya watoto yapewe kipaumbele

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM

SERIKALI kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imeendelea kuimarisha huduma za malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto katika ukanda wa Afrika Mashariki na Afrika, zikiwemo jitihada mbalimbali za kuhamasisha na kufanya ushawishi kwa watoa maamuzi na watunga Sera ili masuala ya malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto yapewe kipaumbele.

Ameyasema hayo Machi 11, 2024 Jijini Dar es salaam Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dorothy Gwajima wakati akisoma hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano wa kimataifa wa malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“imewezesha nchi nyingi Barani Afrika kuwa na Sera na Programu maalum za masuala ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto na Serikali za nchi mbalimbali zimeweza kufanya maamuzi ya kutoa elimu bure katika shule za msingi pamoja na kuanzisha na kuyafanya madarasa ya awali kuwa sehemu ya elimu ya msingi”.

Aidha, baadhi ya nchi za Afrika zimeandaa na zinatekeleza Sera maalum kwa ajili ya Watoto, Mwaka 2016 Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki iliandaa Sera ya Mtoto inayotekelezwa kwa pamoja na nchi za Afrika Mashariki ambayo pamoja na mambo mengine inaelekeza kuimarishwa kwa huduma za malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto.

Pia Hali hiyo imeongeza wigo wa upatikanaji wa huduma za malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto hasa wale wanaoishi katika maeneo ambayo hakuna huduma ya vituo vya kulelea watoto wadogo mchana haipatikani.

Aidha, malezi na makuzi ya watoto kwa sasa yanaathiriwa na changamoto mbalimbali zikiwemo migogoro ya familia ambayo waathirika wakubwa ni watoto, Wazazi au Walezi hawana muda wa kulea watoto wao kwa kuwa busy zaidi na shughuli nyingine na kuacha watoto wanajilea au kulelewa na watu wengine, tunahitaji kutafakari na kuchukua hatua ili kuepukana na baadhi ya vikwazo katika malezi ya watoto wetu.

“tunapaswa kulijadili ni ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano ambao una manufaa mengi lakini pia umekuja na changamoto zake kwa watoto na wazazi au walezi ambapo, watoto wanahusishwa na matumizi yasiyofaa ya mitandao (online platforms) yanayopelekea watoto kufanyiwa ukatili mitandaoni (Online Child Explaitation and Abuse)”.

Hivyo, nasisitiza mila nzuri kwani nyingine zina madhara kwa watoto, Mfano wa Mila yenye madhara kwa watoto ni ukeketaji (Female Genitor Mutilation – FGM), hatupendi kuona watoto wetu wanafanyiwa vitendo hivyo ambavyo vina madhara kwao.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Anna Athanas Paul amesema Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mtu mzima. Mwana mpumbavu ni mzigo kwa mamaye lakini mwana mwenye hekima ni fahari kwa babaye. Kwa hiyo wamama ni jukumu letu kuleta wana wenye hekima

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema kila mtoto ametokana na mzazi ambaye ni Baba na Mama na mtoto huyo anaweza kuwa na mlezi ambaye ni ndugu wa wazazi, kutokana na ukweli huo hakuna jambo linalosababisha kuwepo kwa watoto wanaoitwa wa mtaani kwani hakuna mtaa unaozaa watoto.