May 24, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TTB yamkaribisha Terence kwa ziara ya Utalii wa Michezo

Na Mwandishi wetu,Timesmajira

Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ephraim Mafuru, amemkaribisha nchini kwa mara ya kwanza bingwa wa masumbwi duniani, Terence Crawford, ambaye katika historia yake hajawahi kupoteza pambano lolote.

Ziara hiyo ya wiki moja nchini imeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuendeleza utalii wa michezo nchini.

Akizungumza Mei 24,2026, kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam wakati wa mapokezi ya mwanamasumbwi huyo, Mafuru amesema Serikali imeamua kutumia watu mashuhuri wenye ushawishi mkubwa duniani kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia sekta ya utalii na michezo.

Amesema lengo la kampeni hiyo ni kukuza utalii wa michezo sambamba na kupata idadi kubwa ya watalii wanaoingia nchini na kuongeza muda wa kukaa kwao.

Mafuru ameeleza kuwa mbali na utalii wa wanyamapori, fukwe, utamaduni na mikutano, Serikali sasa imejikita pia katika kuimarisha utalii wa michezo kama bidhaa nyingine muhimu ya utalii.

Katika ziara hiyo, Crawford anatarajiwa kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro kwa lengo la kujionea vivutio vya Tanzania na kuvizungumza katika majukwaa ya kimataifa.

Akizungumzia ujio wake mwana masumbwi huyo ambaye ni raia wa Marekani amesema anafurahi kupata ziara ya wiki moja kujionea utalii na shughuli mbalimbali za michezo akiwa