Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online-Dar
Kwa Mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA), imeeleza kuwa vipindi vifupi vya mvua kubwa inatazamiwa katika mikoa ya Arusha,Kilimanjaro,Manyara Rukwa,Songwe ,Mbeya ,Iringa ,Njombe ,Morogoro,Lindi,na Mtwara.
Ambapo TMA imesema Visiwa vya Unguja na Pemba ,Mikoa ya Dodoma,Singida ,Tanga, Dar-es-Salaam,Kigoma ,Tabora,Katavi,mikoa ya Pwani ikijumuisha Visiwa vya Mafia,Mikoa ya Geita,Mwanza na Shinyanga,itakuwa na hali ya mawingu mvua ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.
Taarifa hiyo imeeleza mikoa ya Mara na Simiyu,Morogoro,Lindi na Mtwara , Arusha ,Kilimanjaro na Manyara, Rukwa ,Songwe, Mbeya,Iringa,Njombe,na Ruvuma itakuwa na hali ya mawingu mvua na ngurumo katika baadhi ya maeneo na vipindi vifupi vya jua.
Mwisho

More Stories
Maboresho sheria yaongeza ushiriki wa watanzania kwenye migodi
Wizara ya Afya yatoa elimu elekezi huduma za afya
Prof.Kabudi:Tumepiga hatua utoaji huduma za Afya