May 3, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Timu ya maofisa balozi nchi zinazozungumza Kifaransa nchini zashinda

Na David John, TimesMajira Online, Dar es Salaam

Timu ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania hususani wanaozungumza lugha ya Kifaransa wamefanikiwa kutwaa kombe na medani baada ya kuifunga timu ya wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Mchezo huo umechezwa kwenye viwanja vya Jakaya Kikwete (Jk Park) Mmazi Mmoja ikiwa ni Tamasha la kimichezo la kusherekea wiki ya Francophonie na timu ya mabalozi kunyakuwa ubingwa.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo Ofisa na Msaidizi wa Balozi wa D.R. Congo, Nadhège Bini Kitenga amesema amejisikia vizuri kushiriki katika tamasha hilo na kufanikiwa kunyakuwa kombe na medani.

Amesema kupitia tamasha hilo yeye kama mwakilishi kutoka Ubalozi wa Congo ikiwa ni sehemu ya nchi inayozungumza lugha ya kifaransa amejifunza mengi wameweza kubadilishana tamaduni za nchi zao.

“Nawashukuru wizara ya Mambo ya nje ya Tanzania kushiriki nasi na hii ndio maana halisi ya ushirikiano na pia inaleta hamasa katika kujifunza na kuzungumza lugha ya kifaransa “amesema Nadhege Bini Kitenga

Akizungumzia nchi zinazozungumza lugha ya kifaransa na walishiriki tamasha hilo ni pamoja na Senegal, Canada, Switsland, Rwanda, Burundi, Sudan, na nchi nyingine nyingi kama Ufaransa wakiwa na wao kama D.R. Congo.

“Nimejisikia furaha kupata medani hii nasema asante sana wote .asante Tanzania na watu wake “amesisitiza

Naye Mwakilishi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manunuzi amesema wamefarijika kushiriki kwenye tamasha hilo licha ya kufungwa lakini walilazimika kusafiri kutoka Dodoma ili kuungana nao.

Amesema kuhusu lugha ya Kifaransa ni muhimu kujifunza kwasababu ni moja ya kugha kubwa inayozungumzwa duniani na kwa Tanzania wameaza kujifunza kuanzia shule za sekondari na vyuoni huku baadhi wakisoma nje ya nchi.

Ni jambo zuri sana na kwakweli ushirikiano huu uendelee japo sisi bado lazima tuendelee kujifunza lugha nyingi tu sio kifaransa pekee yake.” Amesema

Jumuiya ya balozi zinazozungumza Kifaransa na zenye uwakilishi wao nchini wapo katika wiki ya kusherekea lugha hiyo Francophone ambapo ilizinduliwa siku kadhaa zilizopita chini ya Balozi wa Ufaransa, Nabil Hajloui.

Nadhege Bini Kitenga Ofisa kutoka Ubalozi wa D.r Congo nchini katikati aliyevaa kofia akionyesha Kombe na medani baada ya kuibuka washindi wa Tamasha lililokutanisha timu ya wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Nje