January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tigo watoa zawadi ya milioni kumi kwa washindi promosheni ya lipa kwa simu uWini

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mnamo Novemba 23, 2021, Kampuni ya Tigo, kupitia huduma yake ya Lipa Kwa Simu, ilizindua promosheni ya mwisho wa mwaka inayoitwa Lipa Kwa Simu, uWini, promosheni iliyolenga kuhamasisha wateja wa Tigo pesa kutumia huduma ya malipo ya kidijitali.
Na Leo Januari 13, 2022
Wamekabidhi zawadi ya Pesa Taslim Tsh. Millioni Moja kila mmoja kwa washindi 10 wa Promosheni hiyo

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa Promosheni hii, Afisa Mkuu wa Biashara na Huduma za Kifedha TIGO PESA , Angelica Pesha alisema kuwa, “Promosheni hii ililenga kukuza matumizi ya malipo Kidigitali nchi nzima. Tulidhamiria kuwazawadia wateja wetu waaminifu na ndio maana tupo hapa leo hii kwa ajili ya kuwakabidhi zawadi yao ya pesa taslimi Millioni moja kwa washindi 10 bora wa Promosheni hii


Promosheni ya Lipa kwa Simu uWini imewawezesha wateja wote kulipa kwa urahisi kwa makundi mbalimbali ya wafanyabiashara katika sekta zote kama vile; Sehemu za soko, vituo vya mafuta, migahawa, baa, hoteli, maduka makubwa, maduka ya dawa, maduka ya vifaa na mengine mengi.

“Na leo tutawakabidhi washindi wetu hawa zawadi zao na tunaendelea kuwasisitiza wateja wetu wengine kutumiaaa huduma hii maana tuna mambo mengi mazuri tumewaandalia”
Mteja anatakiwa kufanya yafuatayo

  1. Piga 15001#
  2. Chagua ‘5’ Lipa Kwa Simu,
  3. Chagua “1” Kwa Tigo Pesa
    Au lipa kwa kutumia Tigo Pesa App na ufurahie kufanya miamala kirahisi na salama kwa kutumia simu ya mkononi, Alimalizia Bi. Pesha.

Kwa upande wake mwakilishi wa washindi hao kumi ambao wametoka mikoa Mbalimbali hapa nchini Bwana Yusuph Nehemia Mkazi wa Gongo la Mboto Dar Es Salaaam, amewashukuru sana Tigo Pesa kwa kuamua kuwazawadia wateja wake kupitia Promosheni na kueleza kuwa amefaham promosheni hii kupitia App ya Tigo Pesa , na baada ya hapo aliamasika kufanya miamala mingi kadri awezavyo kwa Lipa na leo ameibuka mshindi.