April 20, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge Bonah awataka wenyeviti Kimanga kushirikiana na Diwani kuleta maendeleo

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

MBUNGE wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli. amewataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Kata ya Kimanga Kushirikiana na Diwani wa Kimanga katika Kuleta maendeleo ndani ya kata hiyo

Mbunge Bonah Kamoli aliyasema hayo Dar es Salaam leo katika kikao cha chama cha Kata ya Kimanga kwa ajili ya kutatua kero na kusikiliza changamoto ndani ya chama cha mapinduzi kikao kilichowashilikisha viongozi wa Wilaya Katibu Wilaya ya Ilala na Mwenezi wa Wilaya Ilala .

“Nawaomba Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wa Kata ya Kimanga kukaa meza moja na Diwani wenu katika kuleta maendeleo na kutatua kero za Wananchi”alisema Bonah.

Mbunge Bonah aliwataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wa Kimanga kushirikina na Wananchi na kuitisha vikao kila wakati na kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM ambayo yanatekelezwa na Serikali ya CCM ambayo inaongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassan.

Mbunge Bonah alisema Kimanga maendeleo kwanza uchaguzi mkuu wa 2020 umeisha amewataka wana CCM kushirikiana kuleta maendeleo na kuondoa tofauti zao na kuakikisha chama kinashika dola mwaka 2025.

Kwa upande Mwingine Mbunge Bonah ameagiza Afisa Mtendaji wa Kimanga kila baada miezi mitatu awe anasoma taarifa ya utekelezaji wa kata hiyo ili kujadili kwa pamoja na kujua miradi ya maendeleo iliyochaguliwa na kukubaliana na Chama na uongozi wa kata.

Kwa upande wake Katibu wa Siasa na Uenezi Wilaya ya Ilala Saidi Sidde amewataka Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kabla kuitisha mikutano ya Wananchi wawe wanaitisha mikutano ndani ya chama na kuelezea utekelezaji wa Ilani ya chama na kazi anazofanya Rais kuelezea utekelezaji wake ikiwemo miradi ya maendeleo.

Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala Idd Mkoa alisema Kanuni na Miongozo ya Chama cha Mapinduzi inazuia kupanga safu za uchaguzi ndani ya Chama Wilaya ya Ilala yote anaifahamu sio muda wa kupanga safu watakaopanga safu Wilaya ya Ilala ikiwemo Kata ya Kamanga majina yao yatakatwa.

Aidha Katibu wa CCM Wilaya Ilala Idd Mkoa anatarajia kuunda Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi kufatilia changamoto zilizojitokeza Kata ya Kimanga baina ya Uongozi wa Kata na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wanashindwa kushirikiana kwa pamoja katika kuleta maendeleo.

Katibu wa Wilaya ya Ilala Idd Mkoa (Katikati)akiwa katika kikao cha Chama cha Mapinduzi CCM Kata ya Kimanga leo January 12/2022 Kikao hicho kimeandaliwa na Mbunge wa Segerea Bonah Ladslaus Kamoli (kulia)Kushoto Katibu wa CCM Kimanga Salima Kinyogoli
Mbunge wa Segerea Bonah Ladslaus Kamoli akiwa katika ziara Kata ya Kimanga leo January 12/2022
Kukagua miradi ya maendeleo
Mbunge wa Segerea Bonah Ladslaus Kamoli akiwa katika ziara Kata ya Kimanga leo January 12/2022
Kukagua miradi ya maendeleo (Kushoto)Mwenezi wa CCM wilaya ya Ilala Said Sidde(Picha na Heri Shaaban)