April 19, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tigo wafungua duka jipya wilayani Masasi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Kampuni namba moja kwa utoaji wa huduma za Kidigitali nchini Tigo Tanzania imefungua duka jipya katika mji wa Masasi, kuthibitisha uwekezaji wake wa kimkakati katika ukanda wa pwani.

Duka hili likiwa mkabala na mgahawa wa Himo, limefunguliwa ili kutoa matumizi bora kwa wateja kutoka Masasi na miji ya jirani.

Duka hili jipya litatoa simu janja kudumisha utamaduni wa matumizi ya bidhaa za katika kipindi hiki cha mapinduzi ya kidigitali , Intaneti ya Nyumbani pamoja na ubadilishaji wa SIM, Tigo Pesa, huduma za usajili upya wa kibayometriki n.k

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kaimu Ofisa Mkuu wa Mauzo wa Tigo, Uthman Madati alisema “uzinduzi wa duka hilo jipya unaenda sambamba na mkakati wa Tigo wa kuboresha utoaji wa huduma huku ikitimiza ahadi yake ya kuwapatia wateja fursa ya kupata bidhaa bora na huduma kwa urahisi zaidi wilayani Masasi”.

Duka hili jipya lina eneo maalum la matumizi ambapo wateja wanaweza kupata fursa ya kufanya majaribio na kupata uzoefu wa bidhaa mbalimbali za Tigo kama vile simu za mkononi kabla ya kuzinunua.

“Ahadi yetu kwa wateja ni kuwapa huduma za kibinafsi katika duka moja kwa mahitaji yao yote. Kuongezeka kwa mahitaji ya huduma zetu kunatokana na hitaji la wateja kufuata mtindo wa maisha wa kidijitali kote nchini. Mpango wetu ni kutoa masuluhisho jumuishi kama sehemu ya mkakati wetu wa kuendesha ushirikishwaji wa kidijitali katika ukanda huu” alieleza Madati.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Claudia Kitta aliipongeza Tigo kwa dhamira yao ya kuwekeza rasilimali zake ili kuhakikisha wateja wanapata huduma za kiwango cha kimataifa. Ni imani yangu kuwa Tigo itatoa huduma bora kwa wakazi wa Masasi. Tigo inajulikana kwa bidhaa na huduma zake za kibunifu pamoja na uzoefu wake bora wa wateja na sifa hizi zinaifanya Tigo kuwa mtandao wa kipekee.” Alisema Kitta.

Tigo ni mwanzilishi wa uvumbuzi nchini Tanzania. Duka hili ni la 55 sokoni na ni uthibitisho mwingine wa uongozi wa kitengo cha masoko cha Tigo katika utoaji wa ulimwengu mpya wa kidijitali kwa wateja wake.