December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tetesi za soka Ulaya

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

LEEDS United inajaribu kumshawishi kiungo wa Paris St-Germain na Ujerumani Julian Draxler, 26, ajiunge na klabvu hiyo. (RMC Sport – in French)

Mlinzi wa kati raia England, John Stone 26, anajiandaa kubaki Manchester City msimu huu na kupambania nafasi yake kwenye kikosi cha kwanza cha Pep Guardiola. (Telegraph)

Julian Draxler

Beki wa Chelsea na England Fikayo Tomori, 22, anakaribia kutua Everton kwa mkopo wa muda mrefu. (ESPN)

Barcelona iko tayari kufufua tena nia yao ya kumsainisha beki wa Kihispania wa Manchester City Eric Garcia, 19. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Eric Garcia

Leicester City inaonekana kuizidi kete Manchester United kupata saini ya winga wa Bournemouth na Wales, David Brooks, 23. (Manchester Evening News)

Manchester United wako tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya kipa wao Muargentina Sergio Romero, 33, ambapo Aston Villa na Chelsea wanaripotiwa kumtaka. (Express)

United wanafuatilia pia yanayoendelea kuhusu mlinzi wa kushoto Mhispania Sergio Reguilon kwenye klabu yake ya Real Madrid baada ya kuelezwa kwamba nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 yuko sokoni, hata hivyo kipaumbele chao cha kwanza ni kuongeza nguvu safu ya ushambuliaji. (ESPN)

Liverpool wanafikiria kumuuza msimu huu mshambuliaji wa timu ya taifa ya chini ya miaka 21, Rhian Brewster, 20, kwa sharti la kumrejesha tena siku za usoni. (Sky Sports)

Rhian Brewster

Arsenal imepewa ofa ya kumsajili kipa wa Ufaransa Alphonse Areola, 27, kwa mkopo wa muda mrefu kutoka Paris St-Germain. (Mirror)

Aston Villa inataka kukamilisha haraka usajili wa kipa Muargentina Emiliano Martinez, 28 kutoka Arsenal, ili awahi kucheza mechi ya ya kufungua msimu jumapili hii. (Mail)

West Brom wanafikiria kumsajili kwa mkopo wa mshambuliaji wa Watford na English,r Andre Gray, 29. (Mail)

Mshambuliaji wa Sheffield United na Jamhuri ya Ireland Callum Robinson anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya West Brom. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 anajiandaa kutua kwa uhamisho wa kudumu baada ya kujiunga na timu hiyo kwa mkopo mwezi Januari. (Sky Sports)

Emilio Martinez

West Brom na Leeds zimeongeza nguvu kwenye nia yao ya kumsani kwa mkopo kiungo wa Chelsea na England Conor Gallagher, 20. (Mail)

Bournemouth imepeleka ofa ya kumsajili kwa mkopo beki wa Tottenham na Marekani Cameron Carter-Vickers, 22. (Football Insider)

Bournemouth pia inamtaka kumsajili mshambuliaji wa England Tyrese Campbell, 20, kutoka Stoke City. (Express)