April 20, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

TDAP na Sekta Binafsi ya Pakistani waandaa maonesho maalum ya Uhandisi na Afya

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ya Pakistani (TDAP) na Sekta Binafsi ya Pakistani wanaandaa maonesho maalum ya Uhandisi na Afya ya Pakistani kwa Afrika na Jamhuri za Asia ya kati, huko Lahore, Pakistani kuanzia tarehe 25-27 Februari 2022.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hapo jana, Rais wa TCCIA, Paul Koyi amesema Maonesho hayo ya Uhandisi na Afya ya Pakistani (TDAP) yatahusisha bidhaa za Pakistani za Uhandisi Afya (Dawa, vifaa vya tiba na vifaa vya upasuaji)

Bidhaa kubwa zinazooneshwa katika maonesho hayo ni mshine za kilimo na zana za kilimo, mashine za umeme (aina zote) , vifaa vya ujenzi, bidhaa za chuma, vifaa vya usalama (Ikiwa ni pamoja na Madini)

Bidhaa kubwa zinazooneshwa katika maonesho maalum ya Uhandisi na Afya ya Pakistani kwa Afrika na Jamhuri za Asia ya kati ni dawa, vyombo vya upasuaji na vifaa vya tiba, feni na vifaa vya ujenzi (nyumbani na ofisini) magari ikiwa ni pamoja na tingatinga , malori)

Aidha ameongeza kuwa, Bidhaa kubwa zinazooneshwa katika maonesho maalum ya Uhandisi na Afya ya Pakistani kwa Afrika na Jamhuri za Asia ya kati ni Kemikali, marumaru na Madini, simu za mkononi, vipandikizi na vifaa vya kupikia”

Rais huyo amesema, Bidhaa kubwa zinazooneshwa katika maonesho maalum ya Uhandisi na Afya ya Pakistani kwa Afrika na Jamhuri za Asia ya kati ni vifaa vya kuandikia na karatasi,vifaa vya mpira,vyombo vya plastiki,samani, Mavazi,bidhaa za michezo,vyombo vya muziki,vipodizi, Vito na huduma mbalimbali

Aidha Balozi wa Pakistan nchini Tanzania Muhammad Saleem alisema kupitia maonyesho hayo washiriki watanufaika na fursa za uwekezaji na biashara.

Takribani waoneshaji 250 wa Pakistani na wawakilishi wakuu kutoka mashirika husika ya kibiashara watakua wakiandaa maonesho hayo maalum ya Uhandisi na Afya ya Pakistani kwa Afrika na Jamhuri za Asia ya kati