May 21, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Moja ya Transfoma inayotumika kupoza umeme katika kituo cha Mpomvu Mjini Geita

Tatizo la umeme Geita lapata ufumbuzi

Na Mutta Robert,TimesMajira Online,Geita

SHIRIKA la Umeme Nchini (TANESCO) limeanza kusambaza umeme unaotoka kwenye kituo kipya cha kupooza na kusambaza umeme cha Mpomvu Mjini Geita baada ya kuwashwa rasmi jana na Mkuu wa Mkoa wa Geita mhandisi Robert Gabriel.

Mkuu wa Mkoa wa Geita mhandisi Robert Gabriel akiwasha moja ya mtambo wa kituo Cha kupoza na kusambaza umeme cha TANESCO cha Mpomvu Mjini Geita jana kuruhusu umeme huo uanze kusambazwa kwa watumiaji. Picha zote na Mutta Robert

Kituo hicho kinapokea umeme wa msongo wa Kilovoti 220 kutoka Bulyanhulu na kuupoza hadi Kilovoti 33 kwa ajili ya kuusambaza kwa watumiaji mbalimbali.

Kituo hicho kimejengwa kwa gharama ya Bilioni 50 ambacho umeme utakaotoka kwenye kituo hicho utakuwa na uhakika na kumaliza tatizo la umeme katika Mkoa wa Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita mhandisi Robert Gabriel akiwasha kituo hicho, amesema tatizo la umeme katika Mkoa huo limepataiwa ufumbuzi.

Amesema kuwa malalamiko ya wateja wa umeme hasa wawekezaji kwenye sekta ya madini ,viwanda na watumiaji wa kawaida yamepata suluhisho.