April 28, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Tanzania na Canada Kuimarisha Ushirikiano wa Nishati

Na Mwandishi wetu.Timesmajira

Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Canada nchini, Emily Burns kwa lengo la kuimarisha na kuendeleza ushirikiano kati ya Tanzania na Canada katika sekta ya nishati.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo, Aprili 28, 2026, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, viongozi hao walijadili masuala mbalimbali ya kimkakati yanayohusu sekta ya nishati, ikiwemo Ushirikiano katika kuendeleza nishati jadidifu hususan nishati ya jua na upepo, Kubadilishana uzoefu na mafunzo kwa wataalamu wa sekta hiyo, Teknolojia ya uchimbaji wa mafuta na gesi
pamoja Juhudi za pamoja za kukuza na kuimarisha sekta ya nishati kwa manufaa ya nchi zote mbili

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Mafuta na Gesi,